May 17, 2022

Benki ya NMB yashiriki na kudhamini Wiki ya Ubunifu Dodoma


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi,  akitoa maelezo kwa Makamu wa kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman alipotembelea banda la benki hiyo kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Ubunifu (MAKISATU) yanayoendelea jijini Dodoma. (NA MPIGA PICHA WETU).

 
Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameishukuru Benki ya NMB kwa kushiriki na kudhamini maonesho  ya Kitaifa ya Wiki ya Ubunifu, yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia,
kuanzia tarehe 16 mpaka 20 Mei  katika uwanja wa Jamhuri - jijini Dodoma.
 
Aidha, Profesa Mkenda aliongeza kuwa, benki hiyo imekuwa karibu na Wizara hiyo hata katika utoaji wa mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya Diploma mpaka Shahada, hivyo kusaidia wanafunzi wengi kujiunga na vyuo kuanzia mwaka ujao wa masomo.
 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi alimueleza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman alipotembelea Banda la NMB kuwa, NMB inathamini  ubunifu na imekuwa ikiibuka na masuluhisho bora ambayo yamekuwa na manufaa kwa Benki na Sekta ya Fedha kwa ujumla.
 
"Tunathamini sana ubunifu kwani kwa kupitia hiyo, tumewaletea wateja wetu na watanzania kwa ujumla masuluhisho kama Mshiko Fasta, Lipa Mkononi na NMB Pesa Wakala ambazo zinapunguza wingi wa wateja kufika matawini kupata huduma," alisema Mlozi
 
Lakini pia, Nsolo alisema NMB imeandaa fursa maalum kwa wabunifu mbalimbali hususani wa masuluhisho ya kifedha kujaribu suluhishi zao za kiteknolojia kabla ya kuziingiza sokoni.

No comments:

Post a Comment

Pages