May 17, 2022

RAIS SAMIA KUTOA MIL.10 KILA MKOA KWA MACHINGA

Rais Samia Suluhu Hassan.



Na Asha Mwakyonde, Dodoma

RAIS  Samia Suluhu Hassan jana amepiga siku amezungumza na viongozi wa shirikisho la umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) na kusema kuwa amefuatilia changamoto zilizotajwa na Wamachinga hao ikiwa ni pamoja na zile za uendeshaji wa ofisi zao kwa kipindi cha miaka miwili hivyo kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai ofisi ya yake kupitia Tawala za mikoa na serikali za Mitaa  itatoa kiasi cha shilingi milioni 10 kila Mkoa.

Rais Samia amezungumza hayo jana  kwa njia ya simu wakati mkutano wa mafunzo ya Viongozi wa Machinga Tanzania (SHIUMA) ya siku nne ambayo yanaendelea  yenye kauli mbiu isemayo "Machinga ni Fursa  Sahihi ya Kukuza Uchumi wa Nchi yetu",Jijini hapa, amesema lengo la kutoa kiasi hicho cha  fedha ni kuwezesha shughuli za mbalimbali za Wamachinga hao nchini ili wafanye kazi katika mazingira rafiki.

"Nakushukuru Waziri kwa kuwapa  Wamachinga Ofisi katika  jengo la Serikali,nimesikiliza hotuba yao nawahakikishia ushirikiano mzuri na  mazingira mazuri na ifikapo mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai nitatoa milioni kumi kwa Kila  Mkoa,"amesema Rais Samia.

Awali ,Naibu Katibu Mkuu (SHIUMA) Joseph Mwanakijiji ameeleza kuwa kwa sasa wana mahusiano mazuri na serikali jambo linalosaidia Machinga anakuwa na mazingira mazuri na kuhakikisha anapangwa vizuri na kufanya biashara kwa uhuru.

Amebainisha kuwa wana changamoto nyingi ikiwamo  kero ya miundombinu kwa baadhi ya masoko haiko sawa ambayo inawasababishia  kiuchumi kutokufikia  malengo yao pamoja na kuatarisha  afya zao.

"Changamoto nyingine kuwa ni pamoja na stadi za biashara ,makazo bora,umilikishwaji wa maeneo ya machinga, tunaomba kupewa barua ya idhini kuepuka kuondolewa mara kwa mara pindi halmashauri zinapo badili matumizi ya maeneo ambayo tayari tulizashoeleka wa wateja wetu," amesema.

Mafunzo hayo ya Viongozi wa shirikisho la umoja wa Machinga Tanzania yameandaliwa na

Wizara ya Maendeleo ya jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalumu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameandaa mafunzo hayo ya siku nne leo ni kuwajengea uwelewa wa namna ya kufanya biashara zao katika mazingira ambayo yanahusika.

No comments:

Post a Comment

Pages