Na Lucas Raphael, Tabora
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora imewahukumu wa watu wanne wakazi wa nzega mjini kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la mauaji.
Akitoa hukumu hiyo ya mauaji katika kikao cha mahakama kuu kinachoendelea wilayani nzega mkoani Tabora ,Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda hiyo ,Amor Khamis alisema kutokana na ushahidi usioacha shaka uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo kuu imewakuta na hatia ya kuuwa .
Alisema kwamba ushaidi ulitolewa kwenye kikao hicho kinawatia hatiani washitakiwa wote wanne pasipo shaka yoyote hivyo watakuhukumiwa kunyongwa hadi kufa
Jaji huyo alisisitiza jamii kuachana na dhamna ya ushirikina na kujipatia mali kwa njia ya mkato kitendo alichafanyiwa mwanafunzi huyo cha kumkata kichwa chake na kuondoka nacho kinatia simazi kwa jamii na familia Husika .
Awali ya hapo wakili wa serikali kutoka ofisi ya Taifa ya mashitaka wilayani nzega, ukiongozwa na Jenifa Mandago waliiambia mahakama hiyo kuwa kati ya Tarehe 30 Septemba na Octoba 1 mwaka 2015 huko katika eneo la kijiji cha Silimka kata ya Utwigu wilaya ya Nzega na mkoa wa Tabora watu hao wanne wakiwa ni Samweli Maganga,Selemeni Saidi,Paulo Maganga na Juma dorard walimuuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Nzega , Hosamu Abdulhamani kwa kutumia kitu chenye ncha kali ambapo walikitenganisha kichwa cha marehemu huyo na kiwiliwili chake.
Wakili huyo waliongeza kuwa kichwa cha marehemu huyo waliondokanacho ambapo hakikuweza kupatikana mpaka marehemu anazikwa bila kichwa chake.
Mahakama hiyo baada ya kuridhika na upande wa ushahidi mahakama hiyo imewakuta na hatia na kutoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa wakazi hao wote wanne ambao walikuwa ni wakazi wa mtaa wa Uswilu uliopo Nzega Mjini.
No comments:
Post a Comment