Kamisaa wa Sensa ya mwaka 2022, Anna Makinda wakati akifungua mkutano wa Wadau na Mashirika yasiyo ya kiserikali uliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ili kujadili namna ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi uliofanyika leo jijin Dodoma.
Mtakwimu Mkuu wa wa Serikali Dk. Albina chuwa alifafanua jambo katika mkutano wa Wadau na Mashirika yasiyo ya kiserikali uliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ili kujadili namna ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi uliofanyika jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 imeelekeza nguvu katika ngazi ya chini lengo likiwa ni kufanikiwa zaidi kwa kuwa sensa hiyo ndiyo inayotoa dira ya kupanga maendeleo ya nchi.
Hayo yamesemwa na Kamisaa wa Sensa ya mwaka 2022 Anna Makinda Jijini hapa leo Mei,24,2022, wakati akifungua mkutano wa Wadau na Mashirika yasiyo ya kiserikali uliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),ili kujadili namna ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi Makinda amesema kuwa serikali imeweka mkazo kwa sensa hiyo kwa kuimarisha ili iweze kufanikiwa.
Amesema kuwa mafanikio ya sensa hiyo itafanikiwa endepo Mashirika na wadau kutilia mkazo katika utoaji elimu na uhamasishaji kwa wananchi ili wapate uelewa wa kuhesabiwa.
" Serikali inaamini kutokana na upana wa mashirika yasiyo ya kiserikali yana uwezo wa kuhamasisha nakutoa elimu kwa wananchi. Mashirika haya yamekuwa mazuri katika kuchangia shughuli za wadau," amesema Kamisaa huyo.
Naye Mtakwimu Mkuu wa wa serikali Dk. Albina chuwa amesema kuwa serikali haiwezi kupanga maendeleo bila kuwa na idadi ya Watu inayofahamika.
"Hii ni sensa ambayo inaenda kutupa hali halisi ya mwelekeo wa maendeleo. Pia sensa ya mwaka huu inaenda kuungana na ya majengo tutafahamu mazingira ya watu wanaishi vipi," amesema Dk. Chuwa.
Ameongeza kuwa suala la takwimu ni la ushirikishwaji wa watu wote hivyo ndio maana zaidi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali 7000 yameshirikishwa ili yakatoe elimu kwa wananchi.
Awali Mwenyekiti wa baraza la mashirika hayo Dk. Lilian Badi amesema kuwa ofisi ya takwimu imeelekeza nguvu nyingi katika kutoa elimu pamoja na kushirikisha Umma kuunga mkono katika zoezi hilo la ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu.
Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa nchi ina Asasi zisizo za kiserikali ambazo zinaundwa na makundi mbalimbali ambayo ni zaidi ya 700 yamesajiliwa na yanafanya kazi.
" Sisi kama mabaraza tupo wajumbe 30 ambao tunawakilisha mashirika haya 733 yasiyo ya kiserikali, " amesema Mwenyekiti huyo.
Ameongeza kuwa wamejipanga kutumia mitandao yote ya kitaifa, makundi ya kijamii na mtu mmoja mmoja wanaoguswa na kazi za Mashirika hayo.
No comments:
Post a Comment