May 10, 2022

NMB Teleza Kidijitali yazinduliwa Dar

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza Mfanyabiashara wa vitambaa, Juma Hamad (kulia), wakati walipokuwa wakitembea mitaani kuinadi Kampeni ya TELEZA KIDIJITALI kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam, jana. Katika Kampeni hiyo Wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua Akaunti.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza wafanyabiashara wa duka la vipodozi, Hamede Shirima (katikati) na Haruna Masoud, wakati walipokuwa wakitembea mitaani kuinadi Kampeni ya ‘TELEZA KIDIJITALI’ kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam, jana. Katika kampeni hiyo wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Mkononi, NMB Pesa Wakala na kufungua akaunti. (Na Mpiga Picha Wetu).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kulia) wakipeperusha Bendera za NMB kuashiria Uzinduzi rasmi wa kuinadi Kampeni ya TELEZA KIDIJITALI kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam. Katika Kampeni hiyo Wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua Akaunti.

 

NA MWANDISHI WETU

 

BENKI ya NMB imeanza rasmi kampeni ya kuinadi kampeni ya ya Teleza Kidijitali iliyozinduliwa Aprili 11 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dodoma, na sasa ikipelekwa mtaani, kuwaelimisha wateja na wasiokuwa wateja umuhimu wa huduma zilizo chini ya mwamvuli huo, ambazo ni NMB Pesa Wakala, Lipa Namba na Mshiko Fasta.

 

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika NMB Tawi la Tandika Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, ambako Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, aliambatana na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, kuzindua na kisha kuwatembelea wafanyabiashara madukani ili kuwapa elimu zaidi. 

 

 Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Zaipuna alisema ujio wake yeye na viongozi wengine waandamizi wa NMB Makao Makuu na kuungana na wale wa Tawi la Tandika, umelenga kutoa elimu ya kutosha na kuwaingiza Watanznaia wengi zaidi kwenye Sekta Rasmi ya Kifedha ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali ambazo wanazitoa.

 

 “Tuko hapa kunadi huduma zote muhimu zilizo kwenye mwamvuli wa Teleza Kidijitali, ambazo ni Mshiko Fasta ambayo ni mikopo nafuu isiyo na dhamana, inayopatikana kwa njia ya simu kwa wateja wenye akaunti, ambako mteja hatahitaji kitambulisho wala dhamana yoyote kuupata.

 

 “Pia tumeutumia uzinduzi wa kampeni hii kwa ujumla kunadi huduma ya Lipa Mkononi, ambayo itamuwezesha mfanyabiashara kuitumia kulipwa na wateja wake kwa kutumia namba ya malipo au kuskani QR, huku ikitupa sisi kumbukumbu na historia ya mfanyabiashara ambayo itasaidia hata katika utoaji wa mikopo. 

 

 “Pia tumekuja na NMB Pesa Wakala, huduma inayomuwezesha mtu yeyote kuwa wakala bila kutumia mashine, ambayo itamuwezesha kutoa huduma za kuweka, kutoa ama kutuma pesa kirahisi kwa kutumia hata simu ya kitochi,” alisema Zaipuna, ambaye alishiriki kutembelea wafanyabiashara wa eneo la Tandika madukani mwao kutoa elimu na kusikiliza maoni yao.

 

 Zaipuna aliielezea kampeni hiyo kwamba imelenga kuhakikisha wanawapa elimu Watanzania waweze kuwa sehemu ya watumiaji wa huduma za sekta rasmi ya kifedha na kwamba wanaamini NMB Pesa Wakala, Lipa Namba na Mshiko Fasta, vitakuwa chachu ya ukuaji kibiashara na kiuchumi kwa wateja wao kote nchini, ambako wameahidi kuifikisha  Teleza Kidijitali.

 

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, aliwataka wakazi wa kanda yake kuchangamkia Teleza Kidijitali, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bila kusumbuka kwenda matawini, ili kuokoa muda wa kufanya shughuli nyingine za kukua kiuchumi.

 

“Wito wangu kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla, inayojumuisha Zanzibar na mkoa wa Pwani, ni vema wanapofikiria kufungua akaunti, wafanye hivyo na Benki ya NMB, ambako watapata manufaa makubwa na masuluhisho mbalimbali huku tukiwa sehemu ya ustawi wao kibiashara na kiuchumi,” alisisitiza Donatus.

No comments:

Post a Comment

Pages