HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2022

SERIKALI IMETANGAZA AJIRA 205,000 KWA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (SBU),George Simbachawene  wakati akitangaza nafasi za ajira za muda kwa Makarani na Wasimamizi wa zoezi la Sensa.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (SBU), George Simbachawene amesema kuwa wahusika wa mchakato wa ajira za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu, waheshimu na kuzingatia sheria katika kufanya mchujo wa watu wenye sifa zinatakiwa.

Pia amesema kuwa serikali imetoa  nafasi za maombi  205,000 kwa makarani na Wasimamizi wa zoezi hilo la Senza kuanzia leo Mei 5 hadi 19 mwaka huu.

Waziri Simabachawene ameyasema hayo leo Mei 5, 2022, jijini hapa wakati akitangaza nafasi za ajira za muda kwa Makarani na Wasimamizi wa zoezi la Sensa amesema serikali  kuanzia ngazi zote itakuwa makini kusikiliza mahali popote patakapojitokeza changamoto na kuchukua hatua.

Amesema kuwa  katika utaratibu wa ajira za Umma unaangaliwa na kwamba  lazima kuzingatia vigezo vilovyowekwa na atakayefanya upendeleo atakuwa amefanya makosa  sheria hairuhusu mkakati uliowekwa ni kuzingatia mchakato wa ajira ambazo zimewekewa.

Waziri huyo amefafanua kuwa nafasi 205,000 ni kwa nchi nzima na zimegawanyika hivyo  muombaji akipakua kwenye tovuti  ya www.pmo.go.tz,www.tamisemi.go.tz, www.nbs.go.tz kwa upande wa Tanzania Bara  na www.ompr.go.tz, htts://www.tamisemim.go.tz.au www.ocgs.go.tz kwa wale wa Tanzania Zanzabari  ataona nafasi zilivyogawanyika  na majukumu yake.

"Sifa za muombaji awe na umri wa miaka 18 hadi 45 na mwenye afya njema, awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi, awe mtumishi wa Umma au sekta binafi au yoyoye asiye na ajira anaishi katika eneo husika," amesema waziri Simbachawene.

Amefafanua kuwa ajira hizo zitaombwa kupitia mtandao (Online),  na hazitahusisha malipo ya aina  yoyote  kwa muombaji wa ajira  na kwamba mchakato wa kuchambua  maombi ya kazi pamoja na usajili utasimamiwa na kamati maalumu itakayoundwa katika kila ngazi ya Wilaya.

" Usaili utafanyika katika ngazi ya kata kwa nafasi za makarani Wasimamizi wa maudhui na katika ngazi ya Wilaya kwa Wasimamizi wa TEHAMA," ameongeza:

Niwaombe Watanzania wote wenye sifa ambao wanapenda kuomba nafasi za ajira za Makarani na Wasimamizi wa Sensa kufuata utaratibu uliowekwa kikamilifu ili kuomba nafasi hizi," amesema.

Naye Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anna Makinda amesema kuwa  maandalizi ya sensa yamefika zaidi ya asilimia 81 kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa (UN), imepoisha sensa moja inayofuata nia hatua za maandalizi kama ile iliyoisha ya 2012  maandalizi yake yalitakiwa kuanza lakini hii ya mwaka huu Maandalizi yake yameanza 2018.

Kamishna huyo amesema kuwa tayari sensa ya majaribio imeshafanyika na maandalizi mengine na kwamba  Sensa ya mwaka huu ni ya kutumia TEHAMA, na kwamba wameshafika hatua ya kutangaza na waombaji hao watapatiwa mafunzo ya siku 21.

No comments:

Post a Comment

Pages