May 15, 2022

TASAF, Air Tanzania wacheza soka kisomi

Mwamuzi wa kati wa mechi hiyo Kennedy Emmanue (katikati) akiwa na washika vibendera Mussa Mpita (kulia) na Abdul Yusuph (kushoto).
Wachezaji wa timu ya soka ya Air Tanzania (wenye nyeupe), wakimkaba mchezaji wa timu ya TASAF wakati wa mchuano huo.
Wachezaji wa timu ya TASAF, wakiwa mapumziko huku wakimsikiliza mwalimu wa timu yao (kushoto) wakati huohuo Mkurugenzi wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (kushoto).
 

Na Mwandishi Wetu

MECHI ya soka ya kirafiki kati ya timu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Air Tanzania imemalizika kwa watumishi wa timu zote mbili kucheza kistaarabu na kuwavutia watazamaji waliokuwepo uwanjani.

Mchezo huo wa kirafiki uliohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, Ladislaus Mwamanga, umefanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam, umemalizika jioni ya leo Mei 14.2022.

Katika mchezo uliogubikwa na tambo za washangiliaji wa timu zote mbili, ulianza saa 10 jioni ukichezeshwa na mwamuzi Kennedy Emmanuel.

Licha ya kelele za tambo na kushangilia zilizotoka kwa mashabiki wa timu hizo, wachezaji walionesha burudani ya kutosha kwenye mchezo huo.

Baada ya mchezo huo, Mwamanga aliwapongeza wachezaji wote kwa kuonesha kandanda safi lililosheheni burudani huku akiahidi kuwepo kwa mechi za kirafiki za mara kwa mara hasa kwa watechaji wa TASAF.

“Licha ya kukutana kwa muda mfupi mmetufurahisha sana mmecheza vizuri nawapongeza vijana naamini mchezo ujao mtacheza kwa ubora zaidi,” alisema Mwamanga.

Kwa nyakati tofauti wachezaji wa timu hizo walisema ilikuwa mechi iliyoongeza ukaribu wa kindugu nje ya uwanja na kuomba idadi ya mechi hizo iongezeke.

“Ni mechi ya kindugu tumejuana kwa kuwa mwisho wa siku sisi wote ni watumishi wa wananchi licha ya mazoezi pia tumejenga ukaribu miongoni mwetu,” alisema mlinda mlango wa timu ya TASAF, Ramadhani Madari.

“...Naamini tukikutana wakati mwingine kwenye kazi zetu tutakuwa tunajuana, tumekuwa marafiki sasa,” alisema Denis Lazaro mchezaji wa timu ya TASAF.

Manhaji Leonard mchezaji wa timu ya Air Tanzania, alisema mchezo huo umeongeza urafiki na undugu kati yao hasa nje ya uwanja.

No comments:

Post a Comment

Pages