Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka, akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5, 2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia programu yake ya FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknoloji imesema kuwa imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 5.5 katika mwaka wa fedha 2023/2023, lengo likiwa ni kuweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wabunifu nchini.
Pia Sayansi na Teknolojia ya Ubunifu ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa maendeleo na ni nyenzo ambayo ina leta mabadiliko kwa Taifa kupitia wabunifu mbalimbali.
Hayo yamesema leo Mei, 4,2022,jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Eliamani Sedoyeka wakati akifungua Warsha ya siku moja ya waandishi wa habari iliyolenga kuwajengea uwezo katika masuala ya Sayansi na Ubunifu na kuweza kuhamasisha wabunifu katika wiki ya Ubunifu ambayo inatarajiwa kuanza Mei 15 na kilele chake Mei 20 jijini hapa.
Katibu huyo amesema wao kama taifa lazima watende kazi kuendana na nchi zilizoendelea katika masula ya Teknolojia.
"Hadi Sasa serikali imetumia bilioni 2.3 kwa ajili ya kuendeleza wabunifu 200 ambao wameibuliwa na kutambuliwa katika Ubunifu wao na tayari wameshaingizwa katika kanzidata," amesema.
Amesema kuwa wao kama wizara wanatambua, kuibua na kuboresha bunifu mbalimbali na kwamba katika wiki hiyo kutakuwa na utoaji wa toza kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa milioni 5.
Akimkaribisha Mgeni Maalamu, Prof. Sedoyeka, Mkurugenzi wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu kutoka wizara hiyo Prof. Maulilio Kipanyula amesema wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 lengo lake kubwa ni kuhamasisha, kuweka hamasa ya kisayansi na Teknolojia katika masuala ya kazi za Ubunifu kwenye jamii.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wiki hiyo inaazimishwa sambamba na mashindano ya Sayansi na Teknolojia ya ubunifu na kwamba pamoja na kuwa wiki ya Ubunifu wameweza kuhamasisha na tayari wameshahamasisha mikoa 16 katika ngazi mbalimbali za ubunifu.
Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam,Iringa, Mbeya, Tabora, Mwanza, Arusha,Zanzibar, Mara, Dodoma,Kagera, Njombe Kilimanjaro,Morogoro,Mtwara Tanga na Ruvuma.
Mkurugenzi amesema kuwa katika mikoa hiyo wamepanga kuandaa majadiliano lengo likiwa ni kutangaza Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia.
Prof. Kipanyula amefafanua kuwa kitaifa wiki ya ubunifu mwaka 2021/ 2022 inafanyika kuanzia Mei 15 hadi 20 jijini Dodoma ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali na kauli mbinu ni "Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu".
"Wiki hii itakuwa na shughuli mbalimbali za kiubunifu kutakuwa na majadiliano na wadau wabunifu pamoja na serikali kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja ili kuhamasisha matumizi endelevu ya Sanyansi na Teknolojia ya ubunifu kwa ajili ya Maendeleo ya jami na nchi wa ujumla,"amesema.
Pia amebainisha kuwa wanatarajia kuwa na mafunzo ya ubunifu kwa wajasiriamali lengo lao ni kuona ubunifu unakuwa fursa ya kutengeneza ajira kwa vijana na kwamba kutakuwa na maonyesho ya wabunifu kuonyesha kazi zao.
Amesema maandalizi ya wiki hiyo yamefanywa na wizara ya Elimu kwa kushirikiana na taasisi zake kama Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknoloji (COSTECH).
Awali Meneja Programu wa FUNGUO Innovation kutoka Shirika la Maendeleo Development la Umoja wa Mataifa (UNDP), Joseph Manirakiza amesema kuwa katika ulimwengu wa sasa mtu hawezi kufanya mambo yale yale ambayo yana changamoto za wakati uliopo.
"FUNGUO programu yake ni kuwasaidia wale ambao wameshaonyesha mwanga wa Ubunifu wao ambao wapo sokoni ili waweze kuwasaidiawa," amesema Meneja huyo.
Pia ameongeza wanashirikiana na serikali kuangalia ni mazingira gani wezeshi kwa wabunifu ambao wanaanza biashara iwe rahisi na kwamba kupitia program hiyo huwa wanaendesha mijadala.
No comments:
Post a Comment