May 22, 2022

WADAU WA MADINI WAENDELEA KUPIGWA MSASA KUHUSU USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI KUPITIA MAONESHO JIJINI MWANZA

Tume ya Madini, Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini, kampuni za madini, na watoa huduma kwenye migodi ya madini imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini  kupitia maonesho katika Jukwaa la Kwanza la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini
linalohitimishwa leo  jijini Mwanza.
 
Jukwaa hilo la siku tatu linaloambatana na maonesho lililoanza mapema  tarehe 20 Mei, 2022 linakutanishwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wachimbaji wa madini, watoa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mabenki, na watendaji kutoka Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa madini waliotembelea maonesho hayo wamepongeza maonesho hayo na kutaka elimu kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini kuendelea kutolewa katika mikoa mingine nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages