Tume ya Madini, Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini, kampuni za madini, na watoa huduma kwenye migodi ya madini imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini kupitia maonesho katika Jukwaa la Kwanza la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini
linalohitimishwa leo jijini Mwanza.
Jukwaa hilo la siku tatu linaloambatana na maonesho lililoanza mapema tarehe 20 Mei, 2022 linakutanishwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wachimbaji wa madini, watoa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mabenki, na watendaji kutoka Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa madini waliotembelea maonesho hayo wamepongeza maonesho hayo na kutaka elimu kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini kuendelea kutolewa katika mikoa mingine nchini.
May 22, 2022
Home
Unlabelled
WADAU WA MADINI WAENDELEA KUPIGWA MSASA KUHUSU USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI KUPITIA MAONESHO JIJINI MWANZA
WADAU WA MADINI WAENDELEA KUPIGWA MSASA KUHUSU USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI KUPITIA MAONESHO JIJINI MWANZA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment