June 19, 2022

Jeshi la Polisi Kanda Maalum lawashikilia watuhumiwa 396 kwa uhalifu



Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 396 kwa tuhuma mbalimbali za kiuhalifu ikiwemo unyang'anyi wa kutumia silaha, kupanga njama za kufanya uhalifu, wizi wa magari, pikipiki, makosa ya jinai  pamoja na  dawa za kulevya.

Akizungumza na wanahabari jijini humo Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema katika oparesheni iliyoanza Mei 15 hadi Juni 16 mwaka huu walifanikiwa kuwakamata watu wanne kwa kupanga za uhalifu wa unyang'anyi wa kutumia nondo na mapanga.

" Tumewakata watuhumiwa kwa makosa mbalimbali wakituhumiwa makosa ya kiuhalifu yakiwemo ya wizi wa magari, dawa za kulevya, kupanga njama hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," amesema Kamanda Muliro.

Amebainisha kuwa katika oparesheni hiyo Mtuhumiwa Mohamed  Bakari na wenzake 12 wanashikiliwa kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ikiwemo visu na mapanga na kwamba walijeruhi na kupora simu pamoja na laptop.

Kamnda Muliro amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na ulinzi shirikishi wamefanikiwa kuzipata silaha mbili aina ya pistol zikiwa na risasi 43 ambapo ya pili ilikamatwa Mbagala ikifichwa kwenye matuta.

Amesisitiza kuwa katika tukio la uvunjaji wanamshikilia Omari Wilani (42) mkazi wa Buza na wenzake ambapo walikutwa na TV 8 na  Sh 300,000 ikiwa sehemu ya mauzo ya vitu hivyo.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wa wizi wa magari 15 wamekamatwa na vipuri vya mgari kukutwa huku akikbainisha magari  mawili yamepatikana aina ya Suzuki Carry Namba T-617 DRU na Toyota Wish 106 DNV.

Pia amesema watuhumiwa hao wamekutwa  na vipuri vya magari yaliyoiba, site miller 38, vibao vya namba za magari 47, taa za nyuma 14, injini 3 za pikipiki,Rimu za matairi, mlango wa Prado na kadi za usajili wa magari.

Amefafanua kuwa jeshi hilo linamshikilia Thabit Idd na wenzake 24 kwa makosa ya wizi wa pikipiki 17 zilizoibwa katika maeneo mbalimbali ikiwiwemo Gongolamboto na Tabata hivyo walikutwa na Sh Milioni 2.6

Aidha amesema katika msako wamewakamata 216 wakiwa na  dawa za kulevya mbalimbali ikiwemo Bangi kilogramu 212, mirungi kilo 3.5 pamoja na  kete na misokoto ya Bangi na kukazia kuwa jeshi hilo linamshikilia Fatuma Juma na wenzake 80 wakiwa mtambo wa pombe haramu ya Gongo.

Wakati huo huo, jeshi hilo linamshikilia Joshua Kimange (66) kwa tuhuma za kuawiti wataoto wenye chini ya miaka 7 katika eneo la Gongolamboto na Kipunguni na kwamba mtuhumiwa huyo ameshafikishwa katika Mahakama ya Kinyerezi.

Katika hatua nyingine, Kamanda Muliro amesema wanamtafuta Godbless Sawe (47) kwa tuhuma za kumuua mkewe Esther Benito kwa kutumia kitu chenye ncha kali eneo la Kibamba wilayani Ubungo Juni 14 mwaka huu na kwamba baada ya tukio mtuhumiwa alitoroka.

Kamanda Muliro amesema wanamshikilia Frank Barnabas na mwenzake Joshua Shija kwa kujifanya askari polisi ambapo walikuwa wakipita madukani kuomba misaada ya kutengeneza pikipiki za polisi.


No comments:

Post a Comment

Pages