June 15, 2022

MWANAMKE FUNDI SIMU ZA MKONONI AISHUKURU VETA


Muhitimu wa mafunzo ya kutengeneza simu za mikononi kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kipawa Eunice Kavishe  akionyesha moja ya kifaa ambacho anakitumia wakati akitengeneza simu.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


MUHITIMU wa mafunzo ya kutengeneza simu za mikononi kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Kipawa Eunice Kavishe  ameishukuru mamalaka hiyo Kwa kumpatia ujuzi ambayo unamuongezea kipato baada ya kujiajiri mwenyewe.

Akizungumza juzi jijini Dodoma na Habari Mseto Blog  katika maonyesho ya Elimu ya Ufundi na  Mafunzo Stadi Kavishe amesema kuwa amesomea mafunzo ya utengenezaji simu za mkononi ili aweze kujiajiri wenyewe na kuondoa dhana ya kwamba ufunzi huo unawahusu wanaume pekee.

Kavishe ameeleza kuwa baada ya kuhitimu masomo yake amejiajiri  na anafanya shughuli zake katika mtaa wa Agrey na Masasi Kariakoo jijini Dar es Salaam.

" Nipo hapa katika maonyesho haya kuonyesha ni jinsi gani Veta Kipawa inatoa mafunzo ya ufundi stadi. Pia nimekuja hapa kuwahamasisha vijana hasa Wanawake ambao wengine tayari wameshaanza kujifunza mafunzo haya lakini bado hawajarasimisha biashara zao.

Kavishe amewaomba vijana hasa wa kike kujiunga na vyuo vya veta ili wapate mafunzo na kuweza kufanya kazi zao kitaaluma zaidi.

Ameiomba serikali iweze kuwaendeleza zaidi katika fani hizo na kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kupanua wigo wa taaluma yao.

No comments:

Post a Comment

Pages