June 07, 2022

Toyota Genuine Motor Oil kupatikana kwenye Vituo vya Mafuta vya AFROIL


 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kampuni ya Toyota Tanzania Limited katika kupanua wigo wa bidhaa zake zinazoendelea kukua, Kampuni ya Toyota imeingiza sokoni na ‘Toyota Genuine Motor Oil’ chini ya kaulimbiu “mafuta ya injini pekee, ambayo Toyota yako itahitaji milele”

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja wa Vilainishi Toyota Tanzania Anam Mwemutsi amesema Toyota Genuine Motor Oil (TGMO) ndio mafuta ya injini pekee ambayo yameundwa kwa kuzingatia gari la mteja ambapo tofauti na chapa zingine za vilainishi, TGMO imetengenezwa kisayansi na kujaribiwa kwa uthabiti ili kuhakikisha ulinganifu bora zaidi kwa mahitaji ya injini za gari.

 Amesema kuwa dhamira ya Toyota Tanzania imekuwa ni kusambaza bidhaa bora, Kuwa na uzoefu bora wa wateja na kutengeneza mtandao Bora wa wateja kupitia AFROIL kama mshiriki wa Toyota ambao pia hua na maadili yanayofanana na Toyota Tanzania , katika kutoa huduma bora nchini.

 Amebainisha kuwa Injini za Toyota zimeundwa kwa hali ya juu , na ina utendaji imara kwa mda mrefu na kwa kiwango cha juu, Ili kudumisha kiwango hicho , inahitajika huduma ifanyike mara kwa mara na kutumia vilainishi bora vinavyoendana na Inhin vilainishi vya hali ya juu viliyoundwa kwa vipimo kamili vya injini vyenye kusaidia chombo cha moto na Kilainishi cha TGMO

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa AFROIL, Lutfi Binkleb amesema AFROIL ni biashara inayomilikiwa na wadau wa nchini Tanzania ; inayotoa huduma zausambazaji wa mafuta nchini Tanzania ikiwa na zaidi ya vituo 20 vya mafuta nchi nzima, na itakuwa miongoni mwa wauzaji wa mafuta reja reja walioidhinishwa na Toyota Tanzania Limited kuuza TGMO katika vituo vyao vyote vya mafuta nchini kote Tanzania.

Amefafanua kuwa  kampuni hiyo ya ndani inayofanya kazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 14, ina furaha kushirikiana na chapa maarufu duniani kama Toyota kupitia vituo vyake vilivyosambazwa katika mikoa yote nchini, na mtandao wetu wa usambazaji unaendelea kupanuka kwa kasi kubwa.

“Muungano huu unatupa fursa ya kuwahudumia wateja wetu vizuri zaidi, kwani sasa vituo vyetu vimekuwa vinatoa huduma tofauti tofauti na uleta urahisi kwa wateja wetu , na pia huduma na bidhaa zote zinapatikana katika sehemu moja. Lengo letu ni kuboresha hali ya matumizi ya wateja wetu kwa kutoa mafuta ya hali ya juu na sasa vilainishi vya ubora vilivyo chini ya paa moja ili kuhakikisha kuwa injini za magari , zinafanya kazi kwa ubora wake.”Amesema Meneja Binkleb.

Hata hivyo amesema TGMO inakuja na manufaa kadhaa kwa injini ya Toyota, ikiwa ni pamoja na ulinzi na huruhusu sehemu za injini kufanya kazi pamoja ili, injini isizidi joto na kushika kasi injini kutoa nguvu nyingi zaidi Uchumi kwa kazi nzuri ya injini, ambayo hupunguza kiwango cha nishati inayopotea na kutoa maili zaidi kwa lita na kupunguza matumizi makubwa ya matengenezo.

Manufaa mengine ni pamoja na Kuegemea: Kilainishi kuweka injini Kuwa safi na kuzuia pete za pistoni kushikamana, Urefu wa maisha:kwa kutenganisha asidi zinazosababisha kutu,na kuhakikisha huondoa kutu kwa ajili ya kukipa maisha marefu chombo chako; Utangamano kwa kutoa imani kwamba injini itafanya kazi vyema katika kila hali ya hewa na kila wakati ukiwa na mahitaji ya kuendesha gari.

No comments:

Post a Comment

Pages