June 21, 2022

SERIKALI YASHAURIWA KUSIMAMIA MATUMIZI YA UMMA SMZ

 

Na Mauwa Mohammed Zanzibar

Kamati ya Baraza la Wawakilishi imeishauri Serikali kusimamia vyema matumizi ya fedha za umma ili watu wote wapate hamasa za kulipa kodi kwa hiyari na hatimaye uwe ni utamaduni wa kulipa kodi bila shuruti.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Baraza, Miraji Khams Waziri, wakati akiwasilisha maoni ya  kamati  ya bajeti ya Baraza la Wawakilishi  kuhusu mwelekeo wa hali ya uchumi mpango wa maendeleo na bajeti ya serikali kwa mwaka 2022/2023.

 Mjume huyo alisema lengo la ulipaji wa kodi kwa hiari litafikiwa pale ambapo hakutakuwa na ubadhilifu katika fedha za umma na ukitokezea wahusika wana wajibishwa bila muhali.

Aidha kamati hiyo imeishauri serikali iweke mkakati  malum wa kufuatilia mapato yanayoweza kupatikana katika sekta ya mawasiliano kwani serikali hukosa mapato mengi kutoka katika sekta hiyo.

Pia kamati hiyo   imetaka kila mamlaka ya serikali za mitaa kuainisha vyanzo vyake vya mapato kwa uwazi kwani baadhi ya vyanzo vyengine havikusanywi kabisa katika baadhi ya mamlaka ya serikali za mitaa lakini vyanzo hivyo hivyo vinakusanywa na mamlaka za serikali za mitaa nyengine.

Hata hivyo kutokana na mwenendo wa hali ya  dunia  kamati hiyo ya baraza la wawakilishi la Zanzibar imeishauri serikali kubuni mikakati mahsusi ya kukabiliana na mitikisiko ya kiuchumi ya kidunia.

Alifahamisha kuwa mitikisiko hiyo mara nyingi  husababishwa na vyanzo mbali mbali ikiwemo maradhi ya mripuko na vita.


Pia kamati hiyo ilipendekeza kuimarisha huduma za jamii pamoja na kuimarisha mifumo ya kielekroniki ya ukusanyaji mapato ya serikali.

Kudhibiti matumizi ya serikali yasiyokuwa na tija ,kuimarisha utawala bora pamoja na kuinua maslahi ya umma na kutekeleza miradi ya kimkakati.

Aidha kamati hiyo ilisema ili kupatikana ufaniai wa tija katika utekelezaji wa miradi ya kitaifa ni lazma kuwepo na vipaumbele kama vile kwa mwaka 2020/2023  kuliuwepo na vipaumbele vya kitaifa kama vile kusimamia matum.izi sahihi ya ardhi na kupima maemeo yote.

Kikao cha baraza la Wawakilishi mkutano wa saba unaendelea huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar .


No comments:

Post a Comment

Pages