Na Mwandishi Wetu, Mihambwe
KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na uenezi, Shaka
Hamdu Shaka amepongeza ujenzi kituo cha Afya cha Kitama na kuhaidi
kuishauri Serikali kuongeza fedha na kuleta Wataalam ili kituo hicho
kikamilike na kianze kufanya kazi ya kuwahudumia Wananchi.
Shaka
ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara kikazi ambapo aliwasili
eneo la ujenzi kituo cha Afya cha Kitama kilichopo kata ya Kitama,
Tarafa ya Mihambwe na kupongeza ujenzi unaoendelea unaogharimu fedha
Tsh. Milioni 400 fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
"Ninawapongeza
kata ya Kitama kwa utekelezaji huu mzuri ujenzi kituo cha Afya cha
Kitama, ninawahaidi nitaenda kuishauri Serikali iongeze fedha ili kituo
hiki kikamilike vyema na pia kuiagiza Serikali ilete Wataalamu wa Afya
ili huduma ianze kutolewa kwa Wananchi mara moja." Alisema Shaka.
"Sina
mashaka na ninawapongeza sana kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya
uchaguzi wa ujenzi huu mzuri wa Kituo cha Afya cha Kitama, mnafanya
vyema sana Viongozi pamoja na Wananchi." Alisema Shaka.
Kwa
upande wao mamia ya Wananchi waliojitokeza kumuunga mkono Shaka kwenye
ziara hiyo aliyoifanya kwenye kituo cha Afya cha Kitama walimpongeza
Shaka kwa ziara yake hiyo ambayo ameifanya ya kukagua utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi CCM unaofanywa na Serikali.
No comments:
Post a Comment