HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 05, 2022

SHAKA APONGEZA UJENZI KITUO CHA AFYA KITAMA



Na Mwandishi Wetu, Mihambwe


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka amepongeza ujenzi kituo cha Afya cha Kitama na kuhaidi kuishauri Serikali kuongeza fedha na kuleta Wataalam ili kituo hicho  kikamilike na kianze kufanya kazi ya kuwahudumia Wananchi.

Shaka ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara kikazi ambapo aliwasili eneo la ujenzi kituo cha Afya cha Kitama kilichopo kata ya Kitama, Tarafa ya Mihambwe na kupongeza ujenzi unaoendelea unaogharimu fedha Tsh. Milioni 400 fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.

"Ninawapongeza kata ya Kitama kwa utekelezaji huu mzuri ujenzi kituo cha Afya cha Kitama, ninawahaidi nitaenda kuishauri Serikali iongeze fedha ili kituo hiki kikamilike vyema na pia kuiagiza Serikali ilete Wataalamu wa Afya ili huduma ianze kutolewa kwa Wananchi mara moja." Alisema Shaka.

"Sina mashaka na ninawapongeza sana kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi wa ujenzi huu mzuri wa Kituo cha Afya cha Kitama, mnafanya vyema sana Viongozi pamoja na Wananchi." Alisema Shaka.

Kwa upande wao mamia ya Wananchi waliojitokeza kumuunga mkono Shaka kwenye ziara hiyo aliyoifanya kwenye kituo cha Afya cha Kitama walimpongeza Shaka kwa ziara yake hiyo ambayo ameifanya ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM unaofanywa na Serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages