Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizindua ugawaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wa Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Hafla hiyo ilifanyika katika Kijiji cha Chingunduli, Wilaya ya Nachingwea.Kundi la wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali vya upinzi akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ruangwa, Erasmus Libaba, likishangilia baada ya kupokelewa na wana CCM wakiongozwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, katika Kijiji cha Likunja, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi,
Shaka Hamdu Shaka, akiingiza mapokezi ya wanachama wapya kutoka vyama
mbalimbali vya upinzi akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya
Ruangwa, Erasmus Libaba, katika Kijiji cha Likunja, Halmashauri ya
Wilaya ya Ruangwa. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
NA MWANDISHI WETU
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, amesema watanzania wana haki na
huru kuchagua chama gani cha kujiunga nacho ikiwa ni matakwa ya katiba
ya nchi yetu.
Alisema
hayo kwenye mkutano wa shina namba tawi la CCM Likunja, kata ya Likunja
wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambako alipokea zaidi ya wanachama
130, kutoka vyama vya upinzani.
“Tuko
kwenye maridhiano ya kisiasa ya kufanya siasa safi, siasa za maendeleo
na kila mtu yuko huru kwenda Chama chochote anachoona kinamfaa kufanya
siasa na kushiriki maendeleo ya nchi yetu. Niliuliza mara mbili mbili je
hawa wanakuja ccm kwa hiayari yao? nikaambiwa wameamua wenyewe, nami
na wakaribisha sana mmefanya uamuzi wa busara” alisema.
Amesema
wanachama hao wa vyama vya upinzani wamekuja wakati muafaka ambapo Rais
Samia analitibu taifa kwa maridhiano ya kisiasa na kuimarisha
demokrasia nchini.
“
Tunataka siasa za kuvumiliana, siasa za kuheshimiana, siasa za hoja,
siasa na kiungwana” alisema huku akiwa ameshika kadi za vyama vya
upinzani alivyokabidhiwa.
Shaka
alisema vifaa hivyo ni mali ya vyama hivyo kwahiyo atawapelekea
wahusika wazipangie matumizi na kamwe hawezi kubaki nazo kwani haitakuwa
uungwana.
“Ndugu zangu
hizi kadi, bendera, sare na vitabu vya vyama mlikotoka mie
nitawarudishia wenyewe ili wajue watazitumiaje” aliuambia mkutano huo wa
shina.
Wanachama hao
kutoka vyama vya Chadema ,ACT wazalendo na CUF walimkabidhi Shaka, kadi,
bendera, sare, hotuba za wenyeviti wao, na katiba za vyama hivyo.
Aliyekuwa
mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ruangwa. Erasmus Galosi Libaba alisema
wameamua kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na uongozi wa Rais Samia
pamoja na maendeleo yanayopatikana wilayani Ruangwa.
Akiwa
katika siku yake ya mwisho ya ziara ya mkoa wa Lindi, Shaka alitoa
maelekezo kwa mkuu wa wilaya pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Ruangwa kwenda kijiji cha Likunja kuchunguza tuhuma za ufisadi na wizi
zinazowakabili viongozi wa eneo hilo.
“Shida
yenu hapa naijua, sababu nimeambiwa kabla sijafika. kwahiyo
nimemuelekeza mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa CCM wilaya waje hapa
watume vyombo vya kuchunguza na kiongozi atakayebainika achukuliwe hatua
za kinidhamu” alisema na kuongeza
“Chama hiki si Chama cha mafisadi, wezi na matapeli hiyo tusikubali
kukaa na viongozi wenye tamaa na ubinafsi wa kuibia wananchi pamoja na
kukiuka miiko na maadili ya uongozi. Kwahiyo suala hilo nimeshalitolea
maelekezo kwa viongozi wenu wa wilaya niwatoe hofu litafanyiwa kazi kwa
haraka” alisema Shaka na kuamsha shangwe na vigelegele miongoni mwa
wanachama na wananchi waliojitokeza kumsikiliza.
No comments:
Post a Comment