WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji pamoja na kumpongeza Rais Samia kwa kuipatia wizara hiyo zaidi ya asilimia 95 ya fedha ilizoomba katika bajeti yake jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema kuwa wanajenga miradi ya maji ya kimkakati 175 mijini na miradi 1163 vijijini huku akisema wamejipanga na kwamba wakandarasi watakaoende kutekeleza miradi hiyo ni wale wenye uwezo.
Haya ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kikao kazi cha viongozi, Watumishi na wafanyakazi wa wizara hiyo amesema lengo la kikao hicho ni kuona dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.
Waziri Aweso ameongeza kuwa hawatakuwa na kikwazo kwani Wana fedha za kutona na watahakikisha wakandarasi wanalipwa kwa wakati ili waweze kukamilisha miradi hiyo.
Amesema kuwa hiyo ni agenda muhimu wananchi wa mijini na vijijini waweze kupata maji Safi na salama na kwamba moja ya mikakati ambayo waliwekeana kwa wananchi hao ni utekelezaji wa miradi ya maji usianze kusubiri na kutumia muda mrefu.
"Michakato ambayo inayohusiana na michakato ya manunuzi ya maji uanze sasa hivi sio wakandarasi wapatikane Disemba wapatikane Januari,Machi katika mwaka huo mchakato yote ikamilike Sasa hivi ili tunapoingia katika mwaka mpya na bajeti na miradi ianze utekelezaji wake mara moja ," amesema waziri Aweso.
Amesema kuwa hakuna sababu ya miradi ya maji kutumia muda mrefu na wanatambua miradi hiyo inahitaji Mkandarasi mwenye uwezo apatikane kwa wakati ili ianze utekelezaji wake
Amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya maji inategemea fedha na kwa namna ya kipekee wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha zaidi ya asilimia 95 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Waziri huyo ameongeza kuwa wao kama viongozi wanaahidi kama wizara hawatakuwa na kikwazo kuhakikisha Watanzania waishio mijini na vijijini wanapata huduma maji Safi na salama na yenye kutosheleza.
" Kubwa tulichowaitia hapa waandishi wa habari Leo sisi kama viongozi tumekutana watumishi wetu na wafanyakazi wetu kama kikao kazi kwa ajili ya kujadili bajeti yetu ambayo tumeipitisha, tutumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu na tunamshukuru sana Rais Samia kupitia wizara ya Maji kwa sapoti kubwa ya fedha ambayo imeweza kutusaidia kutekeleza miradi mingine mikubwa vijijini na mjini ambapo wananchi wanapata maji Safi na salama," amesema.
No comments:
Post a Comment