Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na
Makatibu Mahsusi wa Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha
Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika
ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02
Juni, 2022.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama, akimakabidhi cheti Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, kama ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufadhili Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha
Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika
ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, akitoa mada kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT wakati wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha
Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha
Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), wakipata maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT.
Rais Samia
Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha
Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
No comments:
Post a Comment