June 21, 2022

WADAU WAIOMBA SERIKALI KUWEKA MIKAKATI MADHUBUTI YA ELIMU JUMUISHI


Wadau  mbalimbali wa elimu nchini wamebainisha kwamba ili Tanzania iweze kuwa na mfumo wa elimu jumuishi uliobora kunahitajika ufafanuzi wa kina wa kisera na hapo juu walikuwa kwenye mkutano wa kujadiliana hilo.
Wadau  mbalimbali wa elimu nchini wamebainisha kwamba ili Tanzania iweze kuwa na mfumo wa elimu jumuishi uliobora kunahitajika ufafanuzi wa kina wa kisera.

 
Na Fredy Mgunda, Iringa

WADAU  mbalimbali wa elimu nchini wamebainisha kwamba ili Tanzania iweze kuwa na mfumo wa elimu jumuishi uliobora kunahitajika ufafanuzi wa kina wa kisera pamoja na uwepo wa mikakati madhubuti itakayotekelezwa kwa vitendo kwenye aina hiyo ya elimu inayolenga kuwaweka pamoja watoto wenye mahitaji maalumu, kama walemavu, na wale wenye uwezo wa juu kiakili katika ufundishaji na ujifunzaji.

Kwa mujibu wa internews Tanzania Mfumo wa ufundishaji unaolenga kuwasaidia na kuwahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum darasani na utekelezaji kwa vitendo wa utoaji elimu unaowafanya wanafunzi wote kuwa na thamani katika jamii huo ndio Elimu Jumuishi. Internews inataja msingi Mkuu wa elimu hiyo jumuishi kuwa ni utu, ubinadamu wa kuishi pamoja na kushirikiana.

Aidha internews inataja msaada unaohitajika katika elimu jumuishi kuwa ni pamoja na waalimu wenye uelewa mpana dhidi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, utoaji wa msaada kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum, kuwaandaa wanafunzi wasio na uhitaji maalum kuwasaidia na kushirikiana na wanafunzi wenye uhitaji maalumu.

katika kutambua umuhimu wa vyombo vya habari Iringa Development of youth disabled and children care(IDYDC) shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project  unaofadhiliwa na internew Tanzania  katika mkoa wa Iringa kupitia Mratibu wa  mradi Reuben Magayane wanapendekeza jamii ihamasishwe kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto wenye ulemavu,mahitaji maalumu na kuacha tamaduni na imani kuwa watoto wenye ulemavu hawana uwezo na hawastahili kusoma au kujumuika kwenye jamii.

Magayane alisema kuwa sekta ya umma na sekta binafsi washirikiane kuhimiza elimu jumishi  pamoja na  Serikali na wadau wajikite kuondoa vikwazo vilivyopo, serikali iandae mwongozo kwa lugha nyepesi kwa ajili ya wadau wote, wakiwemo walimu wa shule/madarasa .

Alisema kuwa serikali iwekeze katika kuzalisha na kuajiri walimu waliopitia mafunzo ya elimu maalum.” Pamoja na kupitia upya mitaala ya elimu.Pia  kupitia  Taasisi ya Elimu Tanzania serikali  ina wajibu wa kufanya  maboresho ya vitabu vya elimu pamoja na kurekebisha na kujenga miundombinu rafiki ili kukidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu kiujumla

Magayane alesema kuwa kuelekea sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 23 agosti 2022 shirika la IDYDC chini ya mradi wa inclusive media project linatoa rai kwa  Serikali kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu zinazohusu watu wenye ulemavu kwa kuzingatia umri, aina ya ulemavu na jinsi.Lakini pia IDYDC inapenda kuiasa jamii kushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha watu wote wenye mahitaji maalumu na ulemavu hawaachwi nyuma kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu  kwenye zoezi zima la sensa ya watu na makazi kama mwanzo wa kupata mwarobaini wa changamoto zinazowasibu watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu

 

No comments:

Post a Comment

Pages