June 14, 2022

Washindi NMB Bonge la Mpango kuzoa mamilioni

 

Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, B. Neema Kazoviyo akibonyeza kumpigia mmoja wa washindi kumi wa droo ya Bonge la Mpango Awamu ya Tatu, chini ya kampeni ya Teleza Kidijitali ya NMB, kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bi. Irene Kawili pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Gongolamboto, Bw. Demetrius Kugesha wakifuatilia. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Tawi la NMB Gongolamboto jijini Dar es Salaam.

 

NA MWANDISHI WETU

 

MSIMU wa 3 wa Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde iitwayo NMB Bonge la Mpango, inayoendeshwa na Benki ya NMB, umezinduliwa jijini Dar es Salaam Jumatatu Juni 13, ambako Benki hiyo imepanga kuwawekea kiasi cha fedha sawa na salio lililopo katika akaunti kama zawadi kwa wateja watakaoshinda kila wiki, mwezi na Fainali kuu 'grande finale.'

 

NMB Bonge la Mpango msimu huu ni kampeni inayoendeshwa chini ya Programu ya Teleza Kidijitali - mwamvuli unaobeba huduma za NMB Mshiko Fasta, NMB Lipa Namba na NMB Pesa Wakala, hivyo kampeni hiyo mwaka huu itatambulika kama NMB Bonge la Mpango - Teleza na Ushinde.

 

Uzinduzi wa NMB Bonge la Mpango uliofanyika NMB Tawi la Gongolamboto, Dar es Salaam, ulienda sambamba na uchezeshwaji wa droo ya kwanza, ambako wateja 10 waliibuka washindi wa pesa taslimu mara mbili ya kiwango walichonacho kwenye akauti zao (double deposit).

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Mauzo wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Buhatwa Ladislaus, alisema tofauti na misimu iliyopita, msimu huu washindi 10 wa kila wiki, watano wa kila mwezi na watatu wa 'grand finale' watazawadiwa pesa sawa na zilizopo kwenye akaunti zao.

 

Ladislaus alibainisha kuwa, NMB imetenga fedha nyingi zitakazotolewa  kama motisha kwa wateja wapya watakaofungua akaunti na wale wa zamani watakapoweka akiba, sambamba na watumiaji wa huduma tatu zilizo kwenye mwamvuli wa NMB Teleza Kidijitali.

 

"Wito wetu kwa wasio wateja Wetu ni kufungua akaunti na wale wenye akaunti kuweka akiba pamoja na kutumia huduma za NMB Mshiko Fasta, NMB Lipa Namba na NMB Pesa Wakala, ambako droo zitafanyika na watakaoibuka washindi watazawadiwa pesa sawa na kiwango cha akiba kilichomo kwenye akaunti zao," alisema Ladislaus.

 

Naye Meneja wa NMB Tawi la Gongolamboto, Demetrius Kugesha, aliwataka Watanzania kuchangamkia zawadi zitolewazo katika kampeni hiyo ya NMB Bonge la Mpango - Teleza Kidijitali.

 

"Leo tunazindua NMB Bonge la Mpango - Teleza Kidijitali na kuchezesha droo ya kupata  washindi 10 wa kwanza. Hii ni kampeni inayolenga kuhamasisha wateja Wetu kufumisha utamaduni chanya wa kujiweka akiba nankutumia huduma zetu za kibenki," alisema Kugesha.

 

Katika droo hiyo iliyochezeshwa chini ya uangalizi wa Mwakikishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili, washindi 10 waliojishindia pesa taslimu na matawi Yao kwenye mabano ni: Anna Mwalemba (Tunduma) na Mohamed Saadani (Mahenge).

 

Wengine ni pamoja na: Kulangwa Majura (Nansio), Abimelick Nyangwali (Kabanga), Maria Urassa (Nelson Mandela), Huruma Mosha (Ngarenaro), Exaud Mtewele (Kibaha), Emmanuel Zabron (Mihayo), Elisada Kibassa (Mafinga) na Amosi Daudi (Manongo)

No comments:

Post a Comment

Pages