June 01, 2022

WAZABUNI WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI ZA UNUNUZI WA UMMA

 

 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kulia), akimkabidhi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Omolo, Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, jijini Dodoma.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

NAIBU waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande,  amewataka Watumishi wa umma na wazabuni wanaoshiriki katika shughuli za ununuzi wa umma kuzingatia kanuni za ununuzi wa umma na watakao kiuka watachukuliwa hatua stahiki kwa kwenda kinyaume na kanuni za ununuzi wa umma nchini. 

Chande amesema hayo  jijini Dodoma katika uzinduzi wa kanuni za Maadili kwa Watumishi wa umma na Wazabuni wanaoshiriki katika shughuli za ununuzi wa umma ambapo amesema kutozingatia kanuni hizo ni kinyume na kifungu cha sheria 105 cha sheria ya ununuzi wa umma sura 410.


Aidha, Naibu Waziri  Chande amesema  ununuzi wa umma ni eneo muhimu katika matumizi ya fedha za serikali kwa sababu inabeba zaidi ya asilimia 50 ya bajeti ya serikali kila mwaka ambapo mwaka 2021/22 Bajeti ya ununuzi ni shilling Trion 20.48 sawa na Asilimia 56 ya Bajeti yote ya serikali huku Taarifa mbalimbali na Ripoti za kaguzi zinaonesha kuwepo kwa ununuzi unaofanyika kinyume na utaratibu. 

Kwa upande wake katibu Mkuu wizara ya fedha na mipango Emmanuel Tutuba amesema kuwa kanuni hizo zitaimarisha maadili katika ununuzi wa umma.


Naye  Kamishina wa sera za ununuzi wa umma Dk. Fredrick Mwakibibga akitumia fursa hiyo kueleza changamoto zinakabili sekta hiyo  ya manunuzi ya umma ikiwemo usimamizi wa mikataba mibovu ya ununuzi na kuingiliwa kiutendaji kada hiyo ya ununuzi wa umma.

No comments:

Post a Comment

Pages