Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
kimeendelea na zoezi la kudahili wanafunzi wakiwa katika banda la Chuo
hicho katika maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Juu yanayoendelea katika
viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ndani ya banda la Chuo hicho pia kuna bunifu mbalimbali zilizoandaliwa na Wanafunzi wa Chuo hicho.
Wanafunzi wa chuo hicho wamekuja na bunifu mbalimbali ikiwemo kifaa maalum cha kumuwezesha mtumiaji wa gesi za majumbani kujua matumizi yake kabla gesi haijaisha, mbunifu wa kifaa hicho Warda Hamduni alisema "Mtumiaji wa gesi anaweza kujua kiwango cha gesi alichotumia". 'Gas Consumption Monitoring System'.
Naye mwanafunzi Yusuf Abass Saleh amekuja na mfumo wa kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli kielektroniki ambapo Meneja au Mmiliki wa Kituo cha mafuta anaweza kujua kiwango cha mafuta kilichouzwa katika kituo chake popote pale halipo.Mfano wa Kituo cha Mafuta kilichofungwa mfumo wa kuuzia kielektroniki.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Yusuf Abass Saleh, akielezea namna Kituo cha kuuzia mafuta kieletroniki kinavyofanyakazi.
Warda Hamduni ambaye ni mbunifu wa kifaa cha kumuwezesha mtumiaji wa gesi za majumbani kujua kiwango cha matumizi yake 'Gas Consumption Monitoring System'.

No comments:
Post a Comment