Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji , Nishati na Madini Joseph Kilang
akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi amewataka
watendaji wote wa wizara hiyo kuwajibika katika kuwahudumia wananchi
kupata huduma ya Maji Safi na Salama, Nishati na Madini ili kuwaondolea
usumbufu wanaoupata katika kupata huduma hizo hasa Maji.
Aliyasema
hayo katika ukumbi wa ZURA wakati akizungumza na watendaji hao kwaajili
ya kuboresha utendaji kazi wa wizara anayoisimamia ili kupunguza
malalamiko ya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Zanzibar.
Alisema
Maji yanaweza kupatikana kila kona ya Zanzibar lakini anashangazwa
kwanini watu hawapati maji huenda kuna watu wanafunga maji kwa makusudi
ili watumia magari kwaajili ya kufanya biashara ya maji huku wananchi
wakiteseka jambo ambalo sio sahihi hata kwa Mwenyezi Mungu.
“Kila
mfanyakazi ndani ya wizara hii akiulizwa nafasi yake ya kazi aseme mimi
nawatumikia wananchi kupata huduma ya maji kwa hiyo mfanyakazi yeyote
atakayemuona mtu anafunga koki ya maji basi atowe taarifa kwa kiongozi
wake haiwezikani watu wakosema maji, Mtu akipiga simu maji yanfunguliwa
ni wazi kama kuna mchezo unachezwa! Suala la maji linaniumiza kichwa”
Alisema Kilangi.
Katibu
Mkuu Kilangi aliwataka watendaji hao kila mmoja kuwajibika katika
majukumu aliyopewa bila ya kusubiri kusukwa na uongozi kwasabau kila
mfanyakazi apewa majukumu yake (Job Description). Alisema kinachohitaji
katika kutekeleza majukumu hayo ni mashirikaina ya karibu ndio
yatakayoleta maendeleo katika wizara hiyo.
Aidha
alimuagiza Mkurugenzi Utumishi na Uandeshaji kufunga mfumo wa alama za
zidole haraka iwezekanavyo ili kuangalia kwa karibu mahuduria wa
wafanyakazi kwani nidhamu inaanza na mahudhuri ya mfanyakaza wakati wa kuingia na kutoka kazini.
“Sitaki
kusubiri ripoti ya makaratasi nitazidiwa akili nataka ikifika mwisho wa
mwezi na print biometric system inioneshe kwa jina mfanyakazi aliingia
saa ngapi kama saa 2.30 au saa 3.00 na muda aliyotoka. Nahao wasio sikia
Mkrugenzi Utumizi watwange barua kama mtu umemwita hataki kusikia mpe
barua, hatukusudii kuharibiana lakini kama mtu hataki kubadilika basi
sheria za utumishi zitumike. Alisema Kilangi.
Naye
Naibu katibu Mkuu Mwanajuma Majid Abdalla alisema kama wanananchi
hawapati huduma ya maji basi wizara hii itakuwa haina uwajibikani hasa
ukiangalia huduma hii ni muhimu sana kwa kila mtu kwani bila ya maji
hakuna mtu atakaweza kuishi.
Alisema wafanyakazi msiridhike ma majibu ya mafundi ya kusema maji hayatoki, bila ya
kueleza sababbu ya msingi kwasababu kunawatu wanancheza na akili za watu utadhani hawajui kama huduma ya maji inathawabu.
No comments:
Post a Comment