July 13, 2022

Hatimaye! Rayvanny Out WCB


Msanii wa kizazi kipya Raymond Shaban Mwakyusa 'Rayvanny' ameiaga rasmi lebo ya WCB Wasafi ambayo alikuwa akifanya nayo kazi zake za kimuziki.
 
"Ni miaka 6 sasa tangu tumeanza kufanya kazi pamoja my team my family WCB Wasafi. Upendo, umoja imekua nguzo kubwa sana kujifunza na tumefanikisha tukiwa pamoja kama team" alisema

Pia  Rayvanny amemshukuru msanii  Diamond Platnumz kwa nafasi aliyompa katika lebo hiyo.

Aidha, kwasasa Rayvanny anaenda kujikita zaidi katika lebo yake ambayo ni Next Level Music, akiwa kama Rais wa lebo hiyo.

Rayvanny alisainiwa na WCB mwaka 2016, na tangu awe chini ya lebo hiyo ameachia ngoma nyingi, ikiwemo album moja.

No comments:

Post a Comment

Pages