Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, amesema kuwa wanayanga wanataka furaha uwanjani na sio ujenzi wa viwanja pekee.
Kauli hiyo ameitoa kwenye Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unaoendelea jijini Dar es Salaam.
"Wagombea watujengee viwanja lakini la muhimu sana ni furaha ya matokeo ndani ya dakika 90 Ligi ya Mabingwa na matokeo mazuri kwenye mechi za kimataifa ndio dhamira yetu kubwa msimu Ujao" alisema Manara.
Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Dk. Mshindo Msolla, alisema anajivunia kukamilisha mchakato wa mabadiliko.
"Najivunia kukamilisha mchakato wa mabadiliko kwa kwakushirikiana na Viongozi wa Kamati ya Ufundi kuanzia leo mimi ni Kiongozi mstaafu na nitabakia kuwa mwana Yanga, naondoka nikiwa nimekamilisha sehemu kubwa ya mabadiliko kwenye klabu yetu" alisema Dkt. Msolla.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Wakili Ally Mchungahela alisema kuwa "Kuna jumla ya matawi 161 na Jumla ya wapiga kura 805 waliofika leo" alisema.
Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara, akizungumza katika Uchaguzi Mkuu wa kbalu hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa yanga wakiwa katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment