July 18, 2022

Matumla, Mwakinyo wa Tunduru watamba kufanya maajabu Songea



 Na Mwandishi Wetu, Tunduru

 

MABONDIA wa ngumi za kulipwa kutoka Tunduru wilayani hapa wametamba kushinda mapambano hayo katika pambano la Pay Back Night linalotarajia kupigwa Songea  Julai 30,  mwaka huu.

 Katika pambano hilo ambalo linatarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea ambapo Matumla Matumla anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Paul Mavisu wa Songea wakati Mohamed Omary ‘Mwakinyo wa Tunduru akitarajia kupanda ulingoni dhidi ya  Ezra Paul.

Matumla Matumla amepema jana mchana kwenye stendi kuu ya mabasi wilayani hapa  mbele ya mashabiki wake alisema kuwa amejipanga kwenda kushinda pambano hilo ambalo anaamini atamchapa mpinzani wake katika raundi ya pili kutokana na maandalizi makubwa anayoendelea kuyafanya.

“Nimejiandaa kushinda dhidi ya Mavisu kwa sababu hatoweza kuvuka katika raundi ya pili, natambua kwamba hii ni fursa kubwa kwangu kucheza katika pambano la kimataifa ambalo litakalofanyika mkoani na ikizingatiwa na tokea wilayani hivyo matarajio ni makubwa,” alisema Matumla.

 Lakini Mwakinyo wa Tunduru alisema kuwa hawezi kumuhofia mpinzani wake Ezra Paul kutokana na kuandaliwa vizuri na makocha wake kuweza kushinda pambano hilo ambapo amemtaka mpinzani wake ajiandae na kupokea kipigo kizito kutoka kwake.

Kwa upande kocha wa mabondia hao, Ally Andonga alisema kuwa amewafua vizuri mabondia wake ili kuweza kushinda mapambano hayo  kutokana na maandalizi yao kufikia asilimia 80 hivyo wanaamini watakuwa kamili kwa kuwapelekea ushindi wa kazi wa Tunduru katika pambano hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages