July 18, 2022

RC MAKALLA AWAONYA WANANCHI WENYE TABIA YA KUVAMIA MAENEO

 Ataka Taasisi na Wananchi kuyalinda maeneo na kuyaendeleza ili yasivamiwe


- Asisitiza Sheria kutumika kuwawajibisha Wavamizi

- Viongozi wa Mitaa watahadharishwa uuzaji wa maeneo yenye migogoro
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewaonya Wananchi Wenye tabia ya kuvamia maeneo ya Taasisi na watu binafsi na kujenga kuacha tabia hiyo Mara moja kwakuwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao Kilichojumuisha Wakuu wa Wilaya, Kamati za ulinzi na usalama, Wakurugenzi, Wastahiki Meya, makatibu tawala, Wanyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata/ Mitaa ambapo amesema Serikali haitowafumbia macho Wananchi watakaovamia maeneo.

Aidha RC Makalla ameelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuweka Mkazo kwenye usikilizaji na utatuzi wa changamoto ya migogoro ya Ardhi.

Pamoja na hayo RC Makalla amezielekeza Taasisi na Wananchi kuyalinda na kuyaendeleza maeneo yao ili yasivamiwe huku akiwataka Wananchi kuhakikisha wanajiridhisha na Nyaraka na taarifa za Serikali ya mtaa kabla ya kununua eneo.


No comments:

Post a Comment

Pages