July 14, 2022

R Kelly amchumbia mrembo licha ya kuhukumiwa miaka 30 jela


Mwanamuziki Robert Kelly 'R Kelly' (55), amemchumbia mchumba yake Joycelyn Savage licha ya  kutegemea Kusota kwa kipindi kirefu gerezani, hii haijawa sababu ya penzi lake la muda mrefu na mrembo huyo kuvunjika.

Kupitia nyaraka za mahakamani zilizodakwa hivi karibuni zinaonesha mwanadada huyo akiweka wazi kuwa amechumbiwa na R-kelly.

Mrembo huyo aliandika barua kwa hakimu Ann Donnelly aliyekuwa anasimamia kesi ya R Kelly akimuongelea kwa mazuri licha ya kukabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono.

Alisema kuwa uhusiano wangu na Robert (R-kelly) ni mzuri, yeye ni kitu bora kilichowahi kutokea kwangu, uungano wetu ni wakipekee sana, na tumezama kwenye penzi, bado ninamsapoti Robert hadi leo kwa sababu ninampenda. alimalizia

Juni 30 mwaka huu jaji Ann Donnelly alimuhukumu msanii huyo miaka 30 jela kutokana na kukutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake.

No comments:

Post a Comment

Pages