Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akionesha upendo kwa kumnywesha maji, mgonjwa Hawa Hassan kutoka Shelui, ambaye amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida wakati |
Wanajumuiya wa Taasisi inayojihusisha na kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima ya Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) wakiwa na bidhaa mbalimbali na vyakula walivyotoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid al-Adha iliyofanyika leo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amewaongoza wanajumuiya wa Taasisi Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) kwa kuwapatia msaada wa chakula na vinywaji wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.
Taasisi hiyo ambayo inajihusisha kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima imetoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid Al-Adha ilyofanyika leo.
Akizungumza kabla ya kutoa msaada huo, Sheikh Nassoro alisema jambo linalofanywa na taasisi hiyo ni jambo jema kwani limejaa ucha Mungu na kila mwanajumuiya hiya malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.
"Hiki mnacho kifanya ni chema mmeacha shughuli zenu, waume zenu, watoto na marafiki badala ya kusherehekea nao sikukuu hii mmeona mje kutoa faraja kwa kuwatembelea hawa wagonjwa kwa kuwaletea chakula na vinywaji hongereni sana na dhawabu yenu mtaipata," alisema Nassoro.
Naye Katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Ramadhani Mtipa alisema kila sherehe za Eid wamekuwa wakiwatembelea wagonjwa na kuwafariji kwa kuwapa chakula, vinywaji na vitu vingine kama saburi na kuwa jumuiya hiya hiyo inaendesha shughuli zake nchi nzima.
Amirat wa Taasisi hiyo Aisha Asi alisema wamekuwa wakitoka msaada wa kuwatembelea wagonjwa, yatima na wale wasio na ndugu kwa kuwapatia msaada wa chakula bila ya kubagua dini na kuwa kazi hiyo wamekuwa wakiifanya asubuhi na jioni.
No comments:
Post a Comment