HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2022

Benki ya NMB yapiga jeki uimarishaji sekta ya utalii


Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (kushoto), akikambidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana (wa pili kushoto), kwa ajili ya ufadhili wa mafunzo kwa wadau wa mnyororo wa thamani kwenye sekta ya utalii. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Tanzania (NCT), Dk. Shogo Mlozi na wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala. (NA MPIGA PICHA WETU).
Maafisa wa NMB wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB PLC mwishoni mwa wiki ilikabidhi hundi yenye thamani ya 20m/- kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kusaidia kukuza uwezo wa sekta ya utalii hapa nchini.

Msaada huo wa benki hiyo unaunga mkono mkakati wa NCT unaolenga kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii kwa lengo la kuboresha ushindani wa sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay alisema benki hiyo imejipanga kuendeles kusaidia maendeleo ya sekta ya utalii kwa kutabua mchango wake katika uchumi wa nchi.

"Benki ya NMB inathamini sana sekta la utalii nchini na kwa kuonyesha hilo, imejikita zaidi katika kuhakikisha shughuli za utalii zinakua nchini.  Leo tunakabidhi shilingi milioni 20 ambazo zitasaidia katika kuwajengea uwezo wadau katika mnyororo wa thamani wa sekta utalii wakiwemo maafisa wa uhamiaji, watoa huduma wa hoteli na sekta ya uchukuzi miongoni mwa wengine. Ni matumaini yetu kuwa programu hii ya mafunzo itakuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya utalii yenye ufanisi na yenye ushindani,” alisema.

Alisema benki yake imejizatiti kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha kwa kuwa na mifumo bora zaidi wa ubadirishaji wa fedha na pia kuimarisha biashara ya kadi ambayo itawezesha watalii kutohangaika wanapofanya manunuzi  na malipo mbalimbali.

Aidha aliongeza kuwa benki hiyo imewekeza kwenye mfumo wakidigitali zaidi utakotumika katikamakusanyo ya Serikali katikanvituo vyote vya utalii ikiwa lengo la kuchangia shuguli za kitalii nchini.

 “Tayari tumeshashirikisha wadau kadhaa katika sekta ya utalii na tumeweka teknolojia ya mashine za kidigitgali POS yaani Point Of Sales kwa kila kituo cha makusanyo na vivutio vya utalii na watalii sasa wanaweza kufanya malipo kwa kutumia Mastercards, Visa au malipo ya Muungano,” aliongeza.

Waziri wa Maliasili na Utalii Pindi Chana wakati wa hafla hiyo aliishukuru benki hiyo na kusema msaada huo umekuja wakati muafaka hasa katikankipindi hiki ambacho Serikali yake imedhamiria kuongeza mchango wa sekta hiyo huku akisema kuwa sekta ya utalii inatoa fursa nyingi katika sekta ya benki na fedha.

"Tuna maeneo mengi ya utalii na sekta ya utalii ina fursa nyingi ambazo bado hazijatumiwa kikamilifu. Sekta hii inaingiza fedha nyingi za kigeni na inaajiri takribani watu milioni 1.6 moja kwa moja na kwa njia nyingine. Nachukua fursa hii kuishukuru Benki ya NMB kwa dhamira yake ya kusaidia sekta hii na kutoa wito kwa watoa huduma wengine wa fedha kuisaidia wizara,” alisema.

Chana alibainisha kuwa Serikali inalenga watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2025 na kuongeza kuwa lengo hilo haliwezi kufikiwa bila kutoa huduma bora.

“Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameshaonyesha nia njema kwa nchi yetu baada ya kuzindua filamu ya ‘Royal Tour’ inayoonyesha vivutio vya utalii wetu vya kipekee. Tumeanza kuvuna matunda ya filamu hiyo na hii inathibitishwa na ongezeko la idadi ya watalii katika miezi ya hivi karibuni. Sasa wadau wote katika sekta ya utalii hawana budi Ila kutoa huduma bora na kipekee na zitakazokumbukwa na watalii daima, "alisema.

Chana alibainisha kuwa Serikali tayari imeshapanga mipango mbalimbali ya sekta ya utalii na tayari inatumia fursa za kujiingiza katika utalii wa mikutano ambao umeonekana kuwa na faida katika nchi zilizoendelea.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa NCT Dk. Shogo Mlozi alibainisha kuwa mpango wa mafunzo ya kimkakati unalenga washiriki 5000 kutoka katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii kutoka mikoa inayojumuisha Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro na Mara.

Alibainisha kuwa chuo hicho kitatoa mafunzo kwa maofisa 700 wa uhamiaji kwa kuwa wao ndio watu wa kwanza na wa mwisho kushirikisha watalii wanaotembelea Tanzania

"Programu hii ya mafunzo inapongeza juhudi za Serikali za kusaidia maendeleo ya sekta na kuifanya iwe ya ushindani. Sisi kama NCT hatuna budi ila kuja na mikakati ya kuhakikisha kuwa watoa huduma wote kwenye sekta hii wanatoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya soko,” Dk. Mlozi alisema.

 

No comments:

Post a Comment

Pages