August 09, 2022

Matukio ya Uchaguzi Mkuu Kenya

 

Mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Amolo Odinga (77) akipiga kura katika Kituo cha Old Kibera kutekeleza haki yake ya kidemokrasia.  
Mgombea Urais wa chama cha Azimio la Umoja, Raila Odinga akiwasalimia wananchi muda mfupi kabla ya kuingia kwenye kituo cha kupigia kura.

William Ruto akipiga kura yake katika Shule ya Msingi ya Kosachei eneo la Sugoi, Kaunti ya Uasin Gishu.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa ameongoza  mkewe Mama Magareth Kenyatta wakati wa zoezi la kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Mutomo Kaunti ya Kiumbu mapema leo.
Mke wa Rais wa Kenya, Mama Margaret Kenyatta akiwa kwenye foleni ya kupiga kura kwenye kituo cha Shule ya Msingi Mutomo Kaunti ya Kiambu.
 
Mkuu wa Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Kenya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kitwete akitembelea Kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Moi kwa ajilli ya zoezi la kuanza kuhesabu kura.

Raia wa Kenya akiwa amembeba ajuza kwa ajili ya kumsaidia kupiga kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Kisian Kaunti ya Kasumu.
Hara walioshindwa kutembelea wamelazimika kubebwa kufika katika kituo cha kupigia kura.
Picha tofauti zikionesha wapiga kura wakiwa katika foleni.


Maafisa wa Uchaguzi wakiwa wamemtoa kwenye foleni ya kupiga kura mwananchi mmoja ambaye jina lake alikufahamika kufuatia kitendo cha yeye kwenda na taulo na mswaki jambo ambalo lililotafsiriwa kama ukosefu wa maadili.
Mwanasiasa Miguna Miguna aliyekimbilia mafichoni nchini Canada akiwa katika ofisi ya balozi ya Kenya nchini humo akiwa anapiga kura.
Kenya inakuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuruhusu raia wake waliopo nje ya mipaka ya Kenya kupiga kura kupitia balozi zao nchi mbalimbali duniani.

No comments:

Post a Comment

Pages