HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 28, 2022

Meena na utabiri mpya Sheria ya Habari


IWAPO Mchakato wa Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Habari, utafanikiwa kama wadau wa habari tunavyotazamia, utaleta msisimko mpya kwenye tasnia ya habari.


Ni kauli ya Nevile Meena, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ameitoa wakati akizungumza na Radio Abood (Abood FM), Morogoro.


Amesema, iwapo mapendekezo hayo yatafanikiwa kwa kiasi chochote kile, tasnia ya habari itainuka upya tofauti na ilivyo sasa chini ya Sheria ya Habari ya Mwaka 2016.


“Iwapo mapendekezo haya yatapita na kuwa sheria hata kama si yote, yataleta athari kubwa katika tasnia ya habari.


“Ni kwa kuwa, sheria ya huduma ya habari ndio mama wa sheria nyingine, hii imeshika pakubwa ndio maana nasema, itarahisisha sheria zingine kubadilishwa,” amesema Meena.


Amesema, ni jambo la kupongeza kwa hatua ambayo serikali imechukua na ilipofika mpaka sasa, kwani yapo ambayo tayari wamekubakiana na wadau wa habari na mengine hawajakubaliana.


“Kama alivyosema mheshimiwa waziri (Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) wakati alipozungumza na BBC.


“Alisema yapo ambayo wameishakubaliana na mazungumzo bado yanaendelea. Sisi tunaamini kuwa, kuna athari chanya itatokea kwenye uandishi wa habari,” amesema.


Amesema, wadau wa habari wameanzisha mchakato huo kwa kuwa, wana nia nzuri na tasnia ya habari na kwamba, serikali imeona nia hiyo ndio maana imeingia kwenye mazungumzo.


“Sisi tuna nia nzuri na mjadala huu na ninaamini tutafika pazuri na kuifanya tasnia ya habari kuwa salama kwa wamiliki wa vymbo vya habari na wanahabari wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Pages