August 05, 2022

Polisi kuendelea kujihimarisha kutoa mafunzo kukabilina na uhalifu mtandaoni

 

 

NA KENNETH NGELESI, MBEYA

 

JESHI la Polisi nchini limesema litaendelea kuwekeza katika elimu ya  teknolojia kwa askari wake ili kukabiliana na wizi wa kimtandao ambao umeonekana kushamiri kwa kadri mabadiliko ya teknolojia.


Akizungumza na Mwandishi wa habari kwenye banda na Jeshi la Polisi kwenye Maonesho ya wakulima nane nane jijini Mbeya Meneja wa Banda la Jeshi la Polisi na Afisa mnadhimu wa Polisi jamii ACP Barnabas Mwakalukwa alisema kuwa wataendelea kuwekeza kwa katika teknologia

 

 ACP Mwakalukwa  alisema kutokana matukio ya uhalifu kimtandao kuendela kushamiri jeshi lihilo limeendelea kutoa elimu na kutoa mafunzo la askari wake kukabiliana na uhalifu huo.

 

Alisema  mbali na kutoa mafunzo kwa askari wake uli kukabiliana na uahalifu wa kimtandao lakaini wamekita kia kutoa elimu hiyo kwa wananchi kwa ujamla kwa kufanya makongamano,mijadala na kwenye maonyesho mbalimbali kama vile nane nane.

 

“Uhalifu wa zamani wizi kutumia nguvu kwa  kuvamia benki, kuvunja nyuma na utekaji wa magari, lakini teknolojia ilivyobadilika uhalifu umehamia mtandaoni, ndio sababu sisi kama jeshi tuliopewa dhamana wa kusimamia usalama wa raia na mali zao tunatoa mafunzo kwa polisi na raia namna ya kukabiliana na uhalifu huu,”alisema.


 

Akizungumzia sababu ya kushiriki Maonesho hayo kwa Jeshi la Polisi itasaidia kufanya tathimini hasa baada ya kupokea maoni kutoka kwa wananchi walifika kwenye banda  kuhusu utendaji kazi katika kamisheni zote za Jeshi la Polisi.

 

Pia, alisema eneo lingine ambalo kwa sasa linakabiliwa na changamoto kubwa ni migogoro ya wakulima na wafugaji hivyo wamewataka wananchi kutumia fursa hiyo ya kupata elimu ili kutambua wajibu na haki zao.

 

Hata hivyo, akizungumzia vitendo vya ukatili, alisema jeshi hilo limejiandaa vema kubwa ni wananchi kuyatumia ipasavyo madawati ya malalamiko na hilo si kwa wanawake na watoto tu bali hata wanaume. 

 

"Kama nilivyosema kuwa jeshi tunakamisheni nyingi moja wapo ni hii dawati la jinsia kwa hiyo tupo hapa kutoa elimu pamoja na kupokea malalamiko hasa masuala ya ukatili wa kijinsia" alisema Mwakalukwa.

No comments:

Post a Comment

Pages