- Asema endapo watakaidi kulipa, 01/11/2022 Serikali itajitoa rasmi katika udhamini na ili hukumu ya Mahakama itekelezwe
- Wananchi 3,881 wamekaidi kulipa fidia
- Ataka Wavamizi wapya waliovamia Kiwanda na eneo la Jeshi la Wananchi Kuondoka Mara moja
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa mwezi mmoja kwa
Wavamizi wa Ardhi ya Kiwanda Cha Wazo kuhakikisha wanapokea Ankara na
kuanza malipo ya fidia kwa mujibu wa makubaliano yaliyokuwa yamewekwa
awali.
RC Makalla ametoa
maelekezo hayo wakati wa kupokea taarifa ya mwenendo wa zoezi la ulipaji
fidia kwa Wananchi wa Chasimba, Chatembo na Chachui ambapo amesema
endapo Wananchi watakaidi agizo Hilo serikali itajitoa rasmi katika
kuwadhamini na kuachia Kiwanda kutekeleza amri ya Mahakama ambayo ni
bomoabomoa.
Aidha RC
Makalla amesema taarifa inaonyesha Kati ya Wavamizi wote 4,070 ni
Wavamizi 39 pekee sawa na Asilimia 9 wamelipa na wanastahili hati, 150
wamelipa ada ya kuomba kupata hati na 3,881 wamekaidi kulipa.
Kuhusu
Wavamizi wapya waliovamia upya eneo la Kiwanda na eneo la Jeshi la
Wananchi, RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
kuhakikisha Wavamizi hao wanaondolewa Mara moja.
Pamoja
na hayo RC Makalla amewahimiza Wavamizi hao kujiadhari na wanasiasa
wanaotumia zoezi Hilo Kama Mtaji wa kisiasa kwakuwa jambo Hilo limekaa
kisheria.
Itakumbukwa
kuwa zaidi ya Wananchi 4,070 walivamia eneo la Kiwanda Cha Wazo ambacho
ni Mmiliki halali wa eneo Hilo na Mahakama ilitoa amri ya kuondoshwa kwa
Wananchi hao Baada ya kushindwa kesi jambo lilowalazimu kuiangukia
Serikali iwasaidie kutafuta muafaka na Baada ya mazungumzo baina ya
Serikali na Kiwanda iliamuriwa walipe kiasi Cha Shilingi 6,419 kwa Mita
za mraba badala ya 40,000 iliyopendekezwa na Kiwanda lakini Cha
kushangaza Wananchi hao wamekaidi kulipa fidia hiyo.
No comments:
Post a Comment