HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 24, 2022

Udahili Awamu ya Pili waanza leo

 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023.  


 
 
Na Mwandishi Wetu

TUME  ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeeleza kukamilika kwa awamu ya kwanza ya udahili ambapo jumla ya waombaji 106,295 wametuma maombi ya kujiunga na vyuo 76 vilivyoidhinishwa kudahili.
 
 
 Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji Prof. Charles Kihampa alisema kuwa waombaji 106,295 wametuma maombi yao katika vyuo 76 vilivyoainishwa kudahili,aidha jumla ya program 757 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na program 724  kwa mwaka 2021 -2022.
 
 
“Vilevile kwa upande wa nafasi mwaka huu kuna jumla ya nafasi 172,168 ikilinganishwa na nafasi 164,901 kwa mwaka uliopita,hii ni ongezeko la nafasi 7,267 sawa na asilimia 4.4 katika program za shahada ya kwanza,’’alieleza Profesa Kihampa.
 
 
Aliongeza kuwa katika awamu ya kwanza ya udahili jumla ya waombaji 75,163 sawa na asilimia 70.71 ya waombaji wote walioomba  udahili wameshapata udahili vyuoni.
 
 
Alisema mwenendo wa udahili wa awamu ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitano  2018-2019  hadi 2022-2023 unaonesha ongezeko kubwa la waombaji ikiashiria ongezeko la wahitimu wa kidato  cha sita na wale wa stashahada.
 
 
Pia alizungumzia suala la waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kwamba wanatakiwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia jana mapaka septemba 6 mwaka huu.kwa kupitia akaunti ya tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).
 
 
Kuhusu kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili tume imetangaza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi  kwa mara ya kwanza kutokana na mbalimbali watumie fursa hiyo kwa kutuma maombi yao kwenye vyuo wanavyovipenda.
 
 
Pia tume imewaelekeza Taasisi za Elimu ya juu nchini kutangaza program ambazo bado zina nafasi .pia imewaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini.


No comments:

Post a Comment

Pages