August 22, 2022

Vijana wamfagilia DC kibaha kwa juhudi za kuhamasisha Sensa


Kikosi cha wachezaji wa timu ya New Generation ambao ni mabingwa wa michuano ya Samia Suluhu Cup wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Sarah Msafiri.

 

Na Victor Masangu, Kibaha

Baadhi ya wanamichezo wa Mpira wa miguu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani amempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Sarah Msafiri kwa kuweza kuona umuhimu wa  kukuza na kuviendeleza vipaji vyao walivyonavyo.

Wachezaji hao wamesema kwamba wamefarijika Sana kuona wameshilikishwa kikamilifu katika michuano maalumu ya kivumbi Cha Samia Suluhu Cup ambapo wameweza kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao.

Walisema kwamba katika Wilaya ya Kibaha vijana wengi wanapenda kushiriki katika mchezo wa kabumbu lakini wakati mwingine wanakosa fursa ya kuonyesha vipaji vyao hivyo juhudi alizozifanya mkuu hiyo wa wilaya ya Kibaha zinatakiwa kuungwa mkono na viongozi wengine.

"Kwa kweli kwa upande wetu sisi Kama wanamichezo wa wilaya ya Kibaha tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mkuu wa Wilaya kwa kutambua umuhimu wa kutushirikisha katika mashindano haya ya Samia Suluhu Cup na kiukweli tumefarijika sana,"walifafanua wanamichezo hao.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya New generation Zakharia Libobe ambao ndio wametawazwa mabingwa katika michuano ya Samia Suluhu Cup amesema kwamba kupitia michuano hiyo wameweza kuhamasika kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika siku ya kesho.

Nahodha huyo alisema kuwa tangu michuano hiyo ianze kutimua vumbi lake la rasmi katika viwanja mbali mbali vilivyopo Wilaya ya Kibaha wanamichezo na wadau wa soka wameonekana kuhamasika kwa kiasi kikubwa kujitokeza katika kuhesabiwa.



Katika hatua nyingine uongozi wa Chama Cha soka Wilaya ya Kibaha(KIBAFA) nao haukusita kutoa shukrani zake za dhati kwa mkuu huyo wa Wilaya kwa kudhubutu kuanzisha mashindano hayo ya Samia Suluhu Cup ambayo yameweza kuleta tija zaidi katika kukuza vipaji na kuhamasisha zoezi la sensa.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha katika kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Rais Samia Suluhu Hassan aliamua kuanzisha mashindano hayo kwa timbu mbali mbali lengo ikiwa ni suala zima la kuhamasisha wanamichezo wote kujitokeza kwa wingi bila kukosa katika sensa ya watu na makazi.

No comments:

Post a Comment

Pages