Kikosi cha wachezaji wa timu ya New Generation ambao ni mabingwa wa michuano ya Samia Suluhu Cup wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Sarah Msafiri.
Na Victor Masangu, Kibaha
Baadhi
ya wanamichezo wa Mpira wa miguu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani
amempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Sarah Msafiri kwa kuweza kuona umuhimu
wa kukuza na kuviendeleza vipaji vyao walivyonavyo.
Wachezaji
hao wamesema kwamba wamefarijika Sana kuona wameshilikishwa kikamilifu
katika michuano maalumu ya kivumbi Cha Samia Suluhu Cup ambapo wameweza
kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao.
Walisema
kwamba katika Wilaya ya Kibaha vijana wengi wanapenda kushiriki katika
mchezo wa kabumbu lakini wakati mwingine wanakosa fursa ya kuonyesha
vipaji vyao hivyo juhudi alizozifanya mkuu hiyo wa wilaya ya Kibaha
zinatakiwa kuungwa mkono na viongozi wengine.
"Kwa
kweli kwa upande wetu sisi Kama wanamichezo wa wilaya ya Kibaha
tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mkuu wa Wilaya kwa kutambua umuhimu
wa kutushirikisha katika mashindano haya ya Samia Suluhu Cup na
kiukweli tumefarijika sana,"walifafanua wanamichezo hao.
Kwa
upande wake nahodha wa timu ya New generation Zakharia Libobe ambao
ndio wametawazwa mabingwa katika michuano ya Samia Suluhu Cup amesema
kwamba kupitia michuano hiyo wameweza kuhamasika kushiriki katika zoezi
la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika siku ya kesho.
Nahodha
huyo alisema kuwa tangu michuano hiyo ianze kutimua vumbi lake la rasmi
katika viwanja mbali mbali vilivyopo Wilaya ya Kibaha wanamichezo na
wadau wa soka wameonekana kuhamasika kwa kiasi kikubwa kujitokeza katika
kuhesabiwa.
Katika
hatua nyingine uongozi wa Chama Cha soka Wilaya ya Kibaha(KIBAFA) nao
haukusita kutoa shukrani zake za dhati kwa mkuu huyo wa Wilaya kwa
kudhubutu kuanzisha mashindano hayo ya Samia Suluhu Cup ambayo yameweza
kuleta tija zaidi katika kukuza vipaji na kuhamasisha zoezi la sensa.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha katika kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na
Rais Samia Suluhu Hassan aliamua kuanzisha mashindano hayo kwa timbu
mbali mbali lengo ikiwa ni suala zima la kuhamasisha wanamichezo wote
kujitokeza kwa wingi bila kukosa katika sensa ya watu na makazi.
No comments:
Post a Comment