September 09, 2022

Jamii yashauriwa kuacha kuwanyanyapaa Watu wenye Matatizo ya Afya ya Akili, Washia watoa huduma za Afya na Matibabu

 


Mkurugenzi wa Taasisi ya Fikra Afya, Shabil Hussein Khalfan akiwa katika banda la taasisi hiyo kwenye Kambi ya Huduma na Matibabu iliyotolewa na Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithasheria kwenye viwanja hivyo.

 

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Jamii imeshauriwa kuacha tabia kuwanyanyapaa watu wenye matatizo ya afya ya akili badala ijenge utamaduni wa kukaa nao karibu kwani wanaweza kupatiwa matibabu wakaishi maisha ya kawaida.

Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Fikra Afya inayojishughulisha na Kupambana na Unyanyapaa uliopo kuhusu Magonjwa ya Akili na Kuelimisha Umma kuhusu Afya ya Akili , Shabil Hussein Khalfan kwenye Kambi ya Huduma za Afya na Matibabu zilizotolewa na Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithnasheri kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Amesema kuwa jamii ianatakiwa kutambua umuhimu wa afya ya akili sawa na ya afya ya kiwiliwili hivyo lazima ijenge tabia ya kujilinda na afya hiyo sio tu ya kiwiliwili pamoja na unyanyapaa kwa wagonjwa wa akili kwani matibabu yapo na wanaweza kuishi maisha ya kawaida.

" Tunajaribu kuilemisha jamii kuwa afya ya akili ni muhimu sawa na afya ya kiwiliwili sio tu kiwiliwili lazima tuwe na tabia ya kujilinda sio tu ya kiwiliwili na tupambane na unyanyapaa wa watu wenye magonja ya akili sio kwamba walijiamulia matibabu yapo na wanaweza wakaishi maisha ya kawaida," amesema Shabil.

Amebainisha kuwa wameamua kutoa huduma mbalimbali kusaidia ubinadamu kwa kuenzi mafunzo ya mhenga wao Imam Hussein aliyefanyiwa ukatili huko Kerbal katika karne ya 61.

Amesisitiza kuwa Imam Hussein alisimama mbele ya watu waliotaka kumkandamiza na kusimama kwa kusema lazima haki ieleweke kwa kuwajali, kuwaheshimu na kuwathamini binadamu na kila mtu ana haki ya kuishi huru ili aweze kujiendeleza.

Ameongeza kuwa watu waliofika kwenye kambi ya macho, kisukari, afya ya akili, presha walipatiwa huduma za vipimo na matibabu na kwamba kulikuwa na kambi ya kukusanya damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Amefafanua kuwa kwenye kambi hizo kulikuwa na shule kwa jina la Imam Hussein iliendeshwa kwa watu waliofika viwanjani hapo ambapo walipatiwa mafunzo na maadili aliyoyasimamia 

Ametoa wito kwa jamii kujali ubinadamu kwa kusaidiana ili iweze kuishi pamoja ili kuendeleza ubinadamu katika dunia kama mafunzo ya Imam Hussein yanavyoelekeza.

No comments:

Post a Comment

Pages