September 23, 2022

MAYELE AWATULIZA WANANCHI KUTETEMA


Na John Marwa

Mshambuliaji Nyota wa kimataifa wa DR Congo Fiston Kalala Mayele amewatoa hofu wanachama, wapenzi na mashabiki wa Klabu yake ya Yanga SC kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL.

Mayele ameyasema hayo ikiwa ni baada ya kuwepo kwa maneno kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Al Hilal ambao inaonekana kama kizingiti kwao kutinga hatua ya makundi.

Unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kutokana na Ubora wa vikosi vya Klabu zote mbili, uwekezaji wa Al Hilal lakini pia Ubora wa mabenchi ya Ufundi yanayoviongoza vikosi hivyo.

Akizungumza na Azam TV Mayele amesema hawana wasisi wala hofu kuelekea mchezo huo kutoakana na ubora wa mchezaji mmoja mmoja na uzoefu walionao katika michuano ya Kimataifa.

"Kuhusu mechi dhidi ya Al Hilal wachezaji hatuna hofu  kabisa, Yanga tuna wachezaji wakubwa waliozoea mechi kubwa na zenye presha kama Bangala, Djuma Shabani, Bernard Morrison, Aziz Ki na wengine.

"Mfano Mimi mechi yangu kubwa ya kwanza kimataifa kucheza nilicheza nikiwa As Vita Club dhidi ya JS Kabylie ya Algeria na Raja Casablanca ya Morocco, watu walijaa sana Uwanjani lakini haikunisumbua" amesema Mayele akizungumza na Azam TV.

Mayele msimu huu ameshafumania nyavu mara 11 katika michezo sita aliyocheza ya kimashindano.

No comments:

Post a Comment

Pages