September 23, 2022

WATOTO WA AFRIK NA AFRIKA YAO QATAR

Na John Marwa

Ikiwa zimebaki siku za kuhesabika kuelekea Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar Afrika itawakilishaa na Mataifa matano yenye makocha wazawa kwa mara ya kwanza.

Historia huandikwa na kuvunjwa lakini hii ambayo Afrika inaenda kuiandika katika makala haya ya Kombe la Dunia 2022 Qatar itaishi vizazi n vizazi.

Ni wazi Afrika ilikuwa kama mtoto wa kambo hata katika maisha yake binafsi maamuzi yake kufanywa na watu baki hasa katika sekta nyeti kama za kuvipngoza vikosi vya Mataifa ya Afrika katika michuano mikubwa kama Kombe la Dunia.

Miongoni mwa Mkocha wenye uwezo, jina na weledi Mkubwa basi Afrika itasimama na kupiga salute kwa Mwamba kutoka Bondeni Pitso Mosimane.


Kijana huyu wa Madiba ametoa yake ya moyoni alipozungumza na BBC Sport Afrika kuhusiana na ushiriki wa timu za afrika katika fainali za mwaka huu huku wazawa wakichukua hatamu ya kuziongoza nchi zao.

"Kuwaamini Makocha wetu wa Afrika ni jambo kubwa sana na inaonesha ukomavu w hali ya juu sana kwa waliofanya maamuzi hayo ya kuwachagua" amesema  Pitso Mosimane.

"Hii sio kampeni dhidi ya Makocha wa kigeni, hapana Bali ni kuwaunga mkono waliofanya maamuzi haya kuchagua makocha wazawa, hii ni hatua kubwa sana ya kufanya vizuri hata World Cup ijayo." Ameongeza Pitso.

Kwa mara ya kwanza tangu Kombe la Dunia lianzishwe mnamo 1930 kutakuwa na makocha wa Afrika wote wakiziongoza timu zao za Taifa katika Fainali za Kombe la Dunia huko Qatar.
Afrika itawakilishw na Mataifa matano ambayo ni Senegal wakiwa na Mwamba Aliou Cissse, Cameroon wakiongozwa na mkongwe Rigiberth Song, Ghana wakiwa na Gwiji Otto Addo, Tunisi wakiwa na Jalel Kadri na Morocco wakiwa na Walid Regragui.

No comments:

Post a Comment

Pages