HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2022

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AIPONGEZA MKURABITA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI CHAMWINO

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Deogratius Ndejembi (katikati) akishuhudia  wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI),, ambaye pia ni Mbunge wa Mbagala, Abdallah Chaurembo (kushoto) akimkabidhi hatimiliki ya ardhi mmoja wa akina mama wakulima wa Kijiji cha Manyemba katika hafla iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa jengo la Masijala lililojengwa na Mpango wa Urasimishaji Raisilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika kijiji hicho.
Ndejembi ameipongeza MKURABITA kwa kusaidia kumaliza migogoro ya Ardhi katika jimbo la Chamwino.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Deogratius Ndejembi, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Mbagala, Abdallah Chaurembo na Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dk. Seraphia Mgembe wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa jengo la Masjala ya Kijiji hicho cha Manyemba.
Baadhi ya wananchi wa Manyemba wakiwa katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na wajumbe wa Kamati ya USEMI.
Mkurugenzi wa Urasimaji wa MKURABITA, Jane Lyimo, akisoma taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo katika kuwajengea uwezo wananchi kupitia urasimishaji ardhi na biashara.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Deogratius Ndejembi akihutubia wakati wa hafla hiyo ambapo aliishukuru MKURABITA KWA URASIMISHAJI WA ARDHI PAMOJA NA KUMALIZA MIGOGORO KATIKA JIMBO HILO.
Mbunge wa Urambo, Margareth Sitta akimkabidhi hatimiliki ya ardhi mmoja wa wakulima wa Manyemba.
Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya USEMI, Dk. Alice Kaijage akikabidhi hatimiliki kwa mkulima.

No comments:

Post a Comment

Pages