HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 07, 2022

Rc Kunenge azitaka halmashauri kuongeza kasi ya mapato

 

Na Victor Masangu,Pwani 

  

MKUU wa Mkoa wa Pwani,alhaj Abubakari Kunenge , ameziagiza halmashauri zote kuhakikisha kwamba wanajikita zaidi katika kukabiliana na kumaliza migogoro ya ardhi kwa lengo la kuwapa fursa wawekezaji kuja kwa wingi katika kuwekeza viwanda.

 

 

Kunenge ametoa Kauli hiyo Wilayani Kibaha ,wakati wa  kikao kazi cha Viongozi wa Mkoa huo kilichohusu  Tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2021/2022, Tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe na ukusanyaji wa mapato.

 

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo wakurugenzi,wakuu wa Wilaya,wakuu wa idara,wakuu wa taasisi mbali mbali za umma pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kujadili na kuweka mipango ya kusaidia ukusanyaji wa mapato.

 

Aidha Kunenge alisema kwamba ni lazima kila kiongozi wa halmashauri husika anapaswa kuona jinsi ya kuwavutia wawekezaji katika maeneo yao ambao wataweza kuleta mabadiliko chanya katika ongezeko la ukusanyaji wa mapato kupitia viwanda vitakavyojengwa.

 

"Hapa nataka kusisitiza sana kwa halmashauri zote kuondoa kabisa changamoto ya kuwepo kwa migogoro hii ya ardhi kwani nina Imani ikitafutiwa ufumbuzi na maeneo yakawa hayana shida lazima kutawavutia wawekezaji kutoka sehemu tofauti,"alifafanua Kunenge

 

 

Mkuu huyo aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kuweka mikakati ya kubuni vyanzo vingine vipya vya mapato ambavyo vitasaidia katika kuongeza kasi ya ongezeko la mapato na sio kutegemea chanzo kimoja.

 

 

"Ni vema kwa Sasa tukabadilika katika halmashauri zetu kwa kuangalia vyanzo vingine vipya vya matapo ndio serikali yetu inavyotaka kupanga bajeti yake  vizuri ili kuweza kuwahudumia wananchi wake ikiwemo kuwapatia miradi ya maendeleo,"alisema Kuenge.

 

Katika hatua nyingine aliwasisitiza viongozi wote wa Mkoa huo kuorodhesha makampuni ambayo yamewekeza biashara zao katika Mkoa wa Pwani ili aweze kufuatilia jinsi ya utaratibu mzima inatumika katika kulipa Kodi ya serikali.

 

 

Nao baadhi ya viongozi waliohudhulia katika kikao hicho walisema kumekuwepo na wimbi la makampuni kwenda mkoani humo kuchimba madini ya mchanga lakini wamekuwa wakikwepa kulipa kodi hivyo kusababisha kupotea kwa fedha za serikali.

 

Aidha mmoja wa wadau hao ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni ameeleza kuwa bado kuna tatizo la ulipaji wa baadhi ya magari yanayotekea Dar es Salaam kwenda kuchukua madini ya kokoto na badala yake hawalipi mapato katika eneo husika hivyo akaiomba serikali kuingilia Kati.

No comments:

Post a Comment

Pages