Ataja kukamilika kabla ya wakati ujenzi wa daraja la Wami ni kielelezo cha uwezo wa serikali ya awamu ya sita
Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa na
viongozi, wana CCM na wataalamu wakipita juu ya Daraja la Wami mkoani
Pwani alipotembelea ujenzi wa daraja hilo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka
Hamdu Shaka akizungumza na viongozi, wana CCM na wataalamu wakati
alipotembelea ujenzi wa Daraja la Wami mkoani Pwani, jana. (Picha zote
na Fahad Siraji wa CCM).
Na Mwandishi Wetu, Pwani
KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka
Hamdu Shaka amesema Chama hicho kinaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa
miradi ya kimkakati inavyoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya
Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema hata baadhi ya watu waliokuwa wakibeza na kutoa kauli za kejeli kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo sasa wameumbuka.
Shaka
ameyasema hayo leo Septemba 18, 2022 baada ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia
89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.
Aidha
amesema jambo la kufurahisha ni kwamba ujenzi wa daraja hilo unakwenda
kuandika historia ya kuwa miongoni mwa miradi michache nchini
iliyokamilika kabla ya muda uliopangwa.
"Wakati
Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na maneno mengi
sana kuhusu daraja hili la Wami na si hili tu bali maneno yalikuwa mengi
Rais Samia hataendeleza mirad hii ya kimkakati, wiki mbili zilizopita
tulikuwa Mwanza, tumeona ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi
unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria. Tumeona ujenzi wa meli MV.
Mwanza unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria na leo niko hapa
daraja la Wami nashuhudia kwa macho yangu, mikono yangu lakini ukisimama
hapa ukiangalia kule mbele unaona namna gani ambavyo Pwani na Tanga
inavyong'ara kupitia daraja hili,” amesema.
Aliongeza
kuwa, fedha zote zimetoka kwa wakati na hivyo ukichukua asilimia 47 na
asilimia 42.2 unapata asilimia 89.2 kati ya hizo kazi kubwa imefanyika
katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa ya Rais Samia Suluhu
Hassan huku akieleza kwamba hapo ndipo unaona namna gani ambavyo
Watanzania wananufaika na kodi zao kwa sababu fedha iliyotoka kwenye
daraja hilo ni ya ndani.
"Hakuna
fedha ya mjomba hakuna fedha ya msaada ni fedha ya watoka jasho wa
Tanzania ndio imefanya kazi hii na mtaalamu alikuwa ananiambia katika
historia ya nchi yetu na mimi nimefuatilia iko hivyo, hili litakuwa
daraja la kwanza kukamilika kabla ya wakati uliokadiriwa, daraja hili
lilikadiriwa litumie miaka minne lakini tutalifungua kabla ya Novemba
ambao tungetegemea kwamba ndio mwezi wa mwisho,” amesema.
No comments:
Post a Comment