September 18, 2022

Simba kimataifa juzi, jana na leo


Moses Phiri akishangilia bao la pili aliloifugia timu yake dhidi ya Nyasa Big Bullets katika mchezo wa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Na Mwandishi Wetu

 

 WEKUNDU wa Msimbazi wameendeleza wimbi la ushidi katika michuano ya Kimataifa baada kuwaondosha Nyasa Big Bullets katika mchezo wa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

Simba waliingia katika mtanange huu wa mkondo wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza uliopigwa wiki moja iliyopita kule nchini Malawi ambako waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mchezo wa leo ulianza kwa kasi ya chini kwa timu zote mbili kiasi cha kuifanya mchezo kupoa hasa kipindi cha kwanza.

Ubora wa mchezaji mmoja mmoja ndani ya kikosi cha Simba umeendelea kuwa mwiba kwa wapinzani wao kiasi cha kuwafanya kupata matokeo.

Nyasa Big Bullets walikuja na mbinu ya kutaka kuzishambulia katikati ya mstari wa ulinzi na viungo wa ulinzi lakini hawakuweza kufua dafu kutokana na ubora wa Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin ambao walikuwa bora kusoma mikimbio ya Nyasa.

Dakika 29 Moses Phiri aliindikia Simba bao la kwanza kwa kumchambua mlinda mlango wa Nyasa Big Bullet akipokea pasi kutoka kwa Clatous Chama.

Kipindi cha pili Nyasa Big Bullet walikuja na mabadiliko kwa kuufungua mchezo na kuongeza kasi ya mchezo, mpango wao ukawazikia hapa.

Simba waliamka na kuwajibu maswali yote waliyoyauliza Nyasa Big Bullet kwani Simba walikuwa wameikamata mechi na kuwachezesha Nyasa kwenye mdundo walioutaka wao.

Moses Phiri aliingia kambani kwa mara nyingine akiunganisha pasi ya Agustin Okrah na kuwalaza Nyasa kwa mabao 2-0.

Ubora wa Simba SC unabali kwenye mpango wa mwalimu Juma Mgunda kwa namna alivyoamua kui kontro mechi.

Mchezaji mmoja mmoja ndani ya Kikosi cha Simba kwa ubora wake wamezidi kuonyesha utofauti wa madaraja yao dhidi ya wapinzani wao.

Simba wanatinga hatua ya awali ya mtoano kwa jumla ya ushindi wa mabao 4 -0 dhidi ya Nyasa Big Bullet.

Kikosi cha Simba kilichoanza. Aish Manula, Esrael Mwenda, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Kibu Denis, Agustin Okrah na Moses Phiri.

No comments:

Post a Comment

Pages