October 05, 2022

KITUO CHA UTAFITI CHA NCHINI UJERUMANI (CRC) CHATUA MZUMBE


Mtafiti Kiongozi wa mradi wa "Future Rular Afrika" Prof. Detlef Müller-Mahn akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William J. Mwegoha akiwakaribisha Watafiti hao waliotembelea Chuo Kikuu Mzumbe.

Watafiti wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, katika kikao cha utambulisho

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William J. Mwegoha (Kushoto) akimkabidhi zawadi Mtafiti Kiongozi wa mradi wa "Future Rular Afrika"

Watafiti wa Mradi wa "Future Rular Afrika" wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  viongozi na watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaotekeleza mradi huo.

Watafiti wa mradi wa "Future Rular Afrika" wa Kituo shirikishi cha Utafiti cha nchini Ujerumani (CRC) wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe na Wabia wanaotekeleza mradi huo Tanzania na Kenya.


Na Mwandishi Wetu


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William J. Mwegoha, amepokea ujumbe kutoka kituo Shirikishi cha Utafiti (CRC) cha nchini Ujerumani,  wafadhili wa mradi wa ‘Future Rural Africa’ unaotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe, kikiwa ni chuo pekee nchini kinachotekeleza mradi huo.

Akizungumza katika kikao maalumu cha utambulisho kilichofanyika leo , ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Kampasi Kuu Morogoro, Mtafiti Kiongozi wa mradi huo  Prof. Detlef Müller-Mahn,  amesema wanafurahia kufanya kazi na Chuo Kikuu Mzumbe, chini ya uratibu wa Dkt. Frank Theobald, ambapo mradi huo umefanikiwa kumaliza awamu ya kwanza, na kuanza utekelezaji wa  awamu pili ya miaka minne (2022 -  2026).

Akielezeka mradi huo, Prof. Detlef amesema, mradi huo umelenga kufanya utafiti wa “maendeleo vijijini na mabadiliko ya kiekolojia”, ambapo matokeo ya utafiti huo yatasaidia mabadiliko ya Sera, kuimarisha na kuboresha maisha ya jamii zinazoishi vijijini.  

Akiwakaribisha chuoni hapo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha, amesema Chuo Kikuu Mzumbe kinatambua mchango mkubwa wa  mradi huo katika maendeleo ya Taifa na kwamba kipo tayari kuendelea kushirikiana na kituo hicho katika maeneo mengine ya utafiti hasa wakati huu ambao chuo kinajiimarisha zaidi na  kujenga uhusiano na Taasisi za kimataifa zinazojishughulisha na tafiti na masuala ya elimu ya juu.

Akitoa dira ya utekekelezaji,  wa mradi huo, Mratibu wa Mradi huo  Dkt. Frank Theobald, amesema awamu ya pili ya Mradi itahusisha utafiti katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Njombe, Pwani, Iringa, Songwe, Dodoma na Mbeya na kwamba kwasasa timu ya watafiti iliyowasili inatembelea maeneo ya utafiti ili kazi hiyo kuanza.

Amesema zipo faida nyingi za mradi huo kwa Taifa, ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanafunzi wa Shahada za Uzamivu na Umahiri watakahusika moja kwa moja na utafiti huo pamoja na kuwapatia wanataaluma fursa mbalimbali za kujiendeleza katika masuala ya Utafiti.

Mbali na Tanzania, nchi nyingine zinazotekeleza mradi huo barani Afika kwa ufadhili wa Kituo Shirikishi cha Utafiti (CRC) cha nchini Ujerumani ni  Kenya na Namibia.

No comments:

Post a Comment

Pages