Na Mwandishi Wetu
NI nyakati chache sana katika maisha ya mchezo wa mpira wa miguu mlindo mlango anakuwa gumzo ama kuchukua nafasi kwenye vichwa vya habari hasa katika zama hizi za Soka la Maabara.
Yawezekana ikawa sababu ya ubora ama udhaifu lakini Soka la kisasa linahitaji walinda mlango ambao ni 'sweper' kwa maana mwenye uwezo wa kuanzisha mashambulizi kwa uwezo wake wa kupiga pasi.
Ni wazi kuna walinda mlango wengi kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara wenye huo ubora lakini katika kupiga pasi basi NBC PREMIER LEAGUE imeshihudia mlinda lango wenye uwezo Mkubwa wa kupiga pasi kushinda wachezaji wengi sana.
Hapa ndipo jina la Djigui Diarra ambaye ni moja ya makipa bora wanaofanya vizuri sana tokea ameingia hapa nchini.
Diarra ni aina ya makipa wa kisasa ambao moja ya silaha yake kubwa ni upigaji wake wa pasi. Makocha wengi duniani kwa sasa wanapendelea sana aina ya makipa ambao wanaweza kuanzisha mipira kwenye eneo la nyuma na kuhusika kwenye utengenezaji wa nafasi.
Diarra amethinitisha hilo juzi kwenye mchezo Ruvu Shooting dhidi ya Yanga SC, Diarra aliweka rekodi kadhaa
Diarra ndiye kipa aliepiga pasi nyingi bila kupoteza (45). Diarra alivunja rekodi ya hapo awali ambayo ilishikiliwa na Aboutwalib Mshery ambapo msimu uliopita alifanya hivyo kwenye mchezo wa Yanga dhidi Polisi Tanzania katika uwanja wa Benjamini Mkapa, katika mchezo huo Aboutwalib Mshery alipiga pasi 45 lakini akapoteza pasi moja tu.
Kabla ya hapo Beno Kakolanya nae aliweka rekodi ya kupiga pasi nyingi, ambapo alipiga pasi 40 zilizokamilika Yanga dhidi ya KMC. Diarra ameweka rekodi pia ya kucheza muda mwingi zaidi nje ya eneo lake ambapo alitumia dakika 70 nje ya eneo lake huku akitumia dakika 20 kwenye eneo lake.
Kwa mujibu wa Kocha Abely takwimu hizi za Diarra ni rekodi mpya kwenye ligi yetu kwa miaka ya hivi karibuni hususani kipindi cha mapinduzi ya kidigital kwenye matangazo ya ligi kuu kwa njia ya runinga.
No comments:
Post a Comment