October 26, 2022

SIMBA QUEENS YALAMBA DODO IKITIMKIA CAF WCL

 



Na John Richard Marwa

Timu ya Wanawake, ya klabu ya Simba SC ' Simba Queens' imeingia kandarasi ya udhamini na kampuni ya kubashiri ya M Bet ambao pia ni wadhamini wakuu wa Klabu hiyo.

Uongozi wa Klabu ya Simba chini ya Mtendaji Mkuu Barabra Gonzalez leo wameingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiriki ya M Bet  wenye thamani ya Tsh. bilioni moja.



"Simba Queens itaanza kutumia jezi zenye nembo ya M-Bet kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake." Kwa mujibj wa taarifa kupitia ukurasa wao wa Instagram.

Wakati wakisaini  kandarasi hiyo kikosi cha Simba Queens kimetua jioni hii Rabat nchini Morocco tayari kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa upande wa wanawake Afrika (CAF WCL).

Simba Queens wametinga hatua hiyo mara baàda ya kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA na kupata tiketi ya kuuwakilisha ukanda huo kwenye Fainali hizo za Ligi ya Mabingwa sambamba na klabu nyingine saba kutoka katika kanda mbalimbali.




No comments:

Post a Comment

Pages