October 03, 2022

TCU yaongeza muda wa udahili wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa program ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2022/2023


TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa udahili wa shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa programu ambazo zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2022/2023.

 

Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk. Kokuberwa Katunzi-Mollel amesema kuwa katika awamu zote tatu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 umekamilika kwa mujibu wa ratiba ya udahili.

 

Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yametangazwa na vyuo husika, waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Tatu na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo, kuanzia leo Oktoba 3 hadi 24 2022 Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Nne na ya mwisho ya udahili inayoanza leo.kwa kutumia namba maalum ya siri walizotumia wakati wa kuomba udahili.

 

Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja imewekwa kwenye tovuti ya TCU baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu za udahili, Tume imepokea maombi ya kuomba kuongezwa muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.


Aidha TCU imetoa utaratibu wa udahili katika awamu ya nne ambapo waombaji wa udahili na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kama ilivyoainishwa katika Awamu ya Nne kwa mwaka wa masomo 2022/2023.


Tume imetoa wito kwa waombaji wa udahili udahili wa Shahada ya Kwanza kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu.

 

TCU imewaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchin


No comments:

Post a Comment

Pages