November 07, 2022

ARSENAL HAIZUILIKI HAIKAMATIKI EPL


Na Mwandishi Wetu

Ukisikia hawazuiliki hawakamatiki ni Arsenal hao, wa moto sana, kuwafunga unahitaji RB ya Polisi tu si vinginevyo.

Arsenal walikuwa timu bora kwa kila kitu kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho . Kasi, uharaka, ubora wa kupiga pasi, kuzuia na hata kushambulia kila kitu kilikuwa upande wao pale Darajani. Sidhani kama Chelsea walikuwa wanaonekana kufunga goli .!

Ufundi wa Zinchenko kupokea mpira kwenye presha ilikuwa muhimu kwa Arsenal kwenye eneo la kwanza kuzima shinikizo lolote lile  kutoka kwa  Chelsea hasa akiungana na Partey kwenye umbo la  3-2 wakati wakianzisha mpira nyuma huku Xhaka na Odegaard wakiwa namba 8 wawili wa juu

Chelsea walikuwa hovyo sana wakiwa na mpira , mipira haikai mguuni vizuri, pasi mkaa za kutosha kuanzia nyuma kwenye kiungo mpaka ushambuliaji, siamini kama kulikuwa na kitu sahihi chochote walifanya vizuri

Potter aliamua kutoka kwenye mabeki watatu na kutumia mabeki wanne  lakini wale viungo wake watatu hawakuwa na ufanisi dhidi ya shinikizo zuri la  Arsenal kwenye mpira,  matokeo yake hata Aubameyang hakupata huduma yoyote nzuri ndani ya eneo la hatari la  Arsenal

Timu hizi mbili leo mipira ya kulenga lango ilikuwa michache sana , na ilihitaji kosa au ufanisi wa hali ya juu kuweka mpira kambani  

Gabriel Jesus hajafunga goli katika mechi 9 mfululizo , lakini jinsi anavyocheza kwa ajili ya timu , mikimbio yake na shinikizo lake kwenye mpira leo imesababisha kona ambayo ilizaa goli

Leo unaweza kutaja takribani wachezaji wote wa Arsenal kwa kucheza vizuri sanaaaaa kuanzia nyuma mpaka mbele ...taja yoyote yule unayetaka na nitakuambia kacheza boli la juu sana

Ukiona Arteta anamuinua Rob Holding ujue shuhuli imeisha , sahau kurudisha goli.

No comments:

Post a Comment

Pages